Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balozi Mahiga akabidhiwa mikoba ya Balozi Mwapachu

Balozi Augustine Mahiga (Kushoto)  Balozi Juma Mwapachu (Kulia)      

Muktasari:

Itakumbukwa kuwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25, Balozi Mwapachu alirudisha kadi ya uanachama wa CCM.     

Dodoma. Balozi Augustine Mahiga ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), kuziba nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Balozi Juma Mwapachu.

Itakumbukwa kuwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliomalizika Oktoba 25, Balozi Mwapachu alirudisha kadi ya uanachama wa CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idris Kikula alisema Balozi Mwapachu alikuwa amemaliza muda wake tangu Septemba 30, mwaka huu.

“Dk Mahiga ameteuliwa tangu mwezi uliopita na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ni mtu mzoefu katika utumishi na amefanya kazi nzuri sana ndani na nje ya nchi, hivyo tunajua ataliongoza vema baraza la chuo ambalo ndicho chombo cha juu cha uamuzi chuoni hapa,” alisema Profesa Kikula.

Pia, alisema Mkuu wa Chuo hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amemuongezea muda wa miezi sita Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala, Profesa Shaban Mlacha aliyekuwa amalize muda wake Desemba 30, mwaka huu. Alisema uamuzi huo unataka kumpa nafasi ili amalizie miradi aliyokuwa ameianzisha ukiwamo wa umeme wa jua.

Profesa Kikula alisema Profesa Mlacha na Naibu Makamu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri, Profesa Ludovick Kinabo walimaliza muda wao mwaka jana, lakini waliongezewa mwaka mmoja.

Alisema utaratibu wa kuwapata watu watakaoziba nafasi hizo mbili ulioanza miezi sita iliyopita, umeshafanyika.

Kwa upande wa mahafali, Profesa alisema jumla ya wahitimu 4,136 wa kada na ngazi mbalimbali watatunukiwa vyeti.

Alisema idadi hiyo imeongezeka ikilinganishwa na ya mwaka jana ambao wahitimu walikuwa 3,949.

Alisema tangu kuanzishwa kwa chuo hicho, idadi ya wahitimu imefikia 26,663.