Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba auwa mke, mtoto wa miezi sita kwa kuwanyonga

Songwe. Jeshi la Polisi Mkoa Songwe linamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Kaloleni katika Wilaya Songwe akituhumiwa kuwauwa mke na mtoto wake mwenye umri wa miezi sita.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amewaambia waandishi wa habari leo Jumatatu Septemba 25 mwaka huu kuwa mtu huyo amewauwa watu hao kwa kuwanyonga shingoni ambapo chanzo cha tukio hilo kinadaiwa ni wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa huyo kumshutumu mke wake kuzaa nje ya ndoa mtoto huyo.

"Waliouawa ni Editha Msokwa (38) na mtoto wake Esther Emanuel (6 miezi)," amesema Ngonyani.

Aidha Ngonyani ametoa taarifa za vifo vya watu wengine wawili katika matukio tofauti ambapo katika tukio la kwanza amemtaja Mwikasiege Mshani (51) mkazi wa Kijiji cha Ikomela wilayani Mbozi kuwa usiku wa kuamkia leo ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso na watu wasiofahamika.

"Chanzo cha mauaji hayo ni kuwania mali kwenye eneo lake la kazi kisha kumchoma kwenye paji la uso kisha kuiba kiasi cha Sh1.8 milioni ambazo zilikuwa kwenye pub ambayo mmiliki wake ni Athanas Ndosite.

Katika tukio jingine, Kamanda Ngonyani amesema limetokea katika Shule ya Sekondari Mlale wilayani Ileje ambapo Mwalimu Benedictor Mwakimyambili (28) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia shuka alilolifunga kwenye kenchi la nyumba anayoishi.

"Chanzo cha kujinyonga ni msongo wa Mawazo ambayo yalisababishwa na maradhi ya mgongo na tumbo ambayo yalikuwa yakimsumbua muda mrefu" amesema Ngonyani.