Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aweso awaombea ajira, cheo wahandisi waliosimamia mradi

Mwanza. Waziri wa Maji,  Juma Aweso amewasilisha ombi kwa Rais Samia Suluhu Hassan la kupandishwa cheo na ajira kwa wahandisi wawili kati ya wanne waliosimamia utekelezaji wa mradi wa maji wa Kyaka-Bunazi ulioko Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Samia kuhutubia umati wa wananchi uliojitokeza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Waziri Aweso ameomba Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (Mwauwasa), Leonard Msenyele athibitishwe kwenye nafasi hiyo aliyoikaimu kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Katika ombi lake, Aweso pia ameomba kibali cha ajira ya mhandisi aliyemtaja kwa jina moja la Lucas aliyefanya kazi ya kujitolea kusimamia utekelezaji wa mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh15.7 bilioni.

"Baada ya kuajiriwa, sisi Wizara ya Maji tunaomba mhandisi Lucas awe meneja wa mradi huu wa Kyaka-Bunazi tukiamini atausimamia vizuri kwa sababu anaufahamu vema," amesema Aweso

Pamoja na motisha ya kuoandishwa cheo na ajira kwa wahandisi hao wawili, Waziri Aweso pia ameahidi kuwa wizara hiyo itawapa wawili hao na wenzao zawadi maalum kwa uzalendo na uwezo walioonyesha wakati wa usimamizi na utekelezaji wa mradi huo wa maji utakaozalisha zaidi ya lita za ujazo molioni 8 kwa siku..

Huku akiwashukuru watendaji na watumishi wote wa Wizara ya Maji kwa kujitolea kufanya kazi kwa bidii kufanikisha utekelezaji wa miradi, Waziri huyo kijana ameahidi kuwa yeye binafsi na wasaidizi wake wote wataongeza kasi kuhakikisha miradi yote inatekelezwa na kukamilishwa kwa wakati kulingana na thamani ya fedha.