Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ATE walalamikia mrundikano wa kodi

ATE walalamikia mrundikano wa kodi

Muktasari:

  • Chama cha Waajiri Nchini (ATE) kimelalamikia mrundikano wa kodi zinazotozwa nchini, wakisema  zimeongeza gharama kwa waajiri.

Dodoma. Chama cha Waajiri Nchini (ATE) kimelalamikia mlundikano wa kodi zinazotozwa nchini wakisema zimeongeza gharama kwa waajiri.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ATE, Jane Nyimbo leo Jumapili, Mei Mosi 2022, katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zinazofanyika katika uwanja wa Jamuhuri jijini hapa.

“Waajiri wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mlundikano wa kodi ambazo wamekuwa wakitozwa na mamlaka mbalimbali na hali hiyo inaongeza gharama ya kufanya biashara kutokana na ugumu katika mazingira ya biashara,” amesema.

Amesema changamoto hiyo imewafanya baadhi ya waajiri kulazimika kupunguza wafanyakazi hasa katika sekta ambazo zimeathiriwa na janga la ugonjwa wa Ukimwi na Uviko-19.

Ametoa mfano wa sekta hizo ni ya ukarimu na utalii.