Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Shoo: Waliomshambulia Dk Kitima hawaitakii mema nchi

Moshi. Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo amelaani kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Dk Charles Kitima akisema ni tukio baya.

“Tukio la kushambuliwa kwa Dk Kitima linashtusha, linasikitisha na linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na Watanzania. Yeyote aliyetenda unyama huu ajue yupo Mungu,”amesema Askofu Shoo akizungumza na gazeti hili leo Mei Mosi, 2025.

“Yeyote aliye nyuma ya uovu huu haitakii mema nchi yetu wala Rais wetu (Samia Suluhu Hassan). Damu za watu hazimwachi mtu salama,” amesema Askofu Shoo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

CCT ni taasisi inayowakilisha Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotestanti na pia inaundwa na makanisa mbalimbali wanachama na vyama vya Kikristo au vyenye mwelekeo wa Kikanisa kutoka Tanzania Bara na visiwani.

“Tuiombee sana nchi yetu na tuyakatae mambo kama haya. Tofauti zitatuliwe kwa njia ya mazungumzo sio kwa kujeruhiana na kuuana,”amesisitiza Askofu Shoo.

Tukio la kushambuliwa kwa Dk Kitima lililotokea usiku wa jana Aprili 30,2025 eneo la Kurasini Temeke, Dar es Salaam, zilipo ofisi za TEC makao makuu, limeibua hisia tofauti miongoni mwa Watanzania wakiwamo viongozi wa dini.