Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Lwiza: Kuzaliwa kwa Yesu ni utimilifu wa unabii

Muktasari:

  • Waumini wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani wamekumbushwa namna maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa Kiongozi wao Yesu Kristo kulivyotimiza unabii

Dar es Salaam. Askofu Msaidizi, Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Chediel Lwiza amesema kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini wa dini ya Kikristo, Yesu Kristo kulikuwa ni kutimia kwa unabii uliotabiriwa na Nabii Mika karne nne kabla ya uzao huo.

Askofu Lwiza ameelezea jinsi tukio la kuzaliwa kwa Yesu lilivyotimiza unabii huo akihubiri katika ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika Kanisa la Azania Front.

Amesema kuwa habari ya Yesu kuzaliwa Bethelehemu haikuwa ya kupangwa na wazazi wake Mariam na Yusufu bali ilikuwa imepangwa na Mungu kuwa atazaliwa mahali hapo.

"Wakati mwingine wazazi wanaweza kuwa wanapanga kuwa huyu mtoto azaliwe wapi lakini Mariam na Yusufu hawakupanga kwamba huyu mtoto tuliyesikia habari zake kutoka kwa malaika (alipompelekea ujumbe Mariam kuwa atachukua mimba kwa uwezo wa Mungu na atamzaa mtoto wa kiume) kuwa azaliwe Bathelehemu", amesema na kuongeza:

"Lakini aliyepanga azaliwe Bethelehemu ni Mungu mwenyewe. Na ndio maana Bethelehemu inatambulika kama nyumba ya mkate na Yesu anatambulishwa kwetu kama mkaye wa uzima".

Amesema Wakristo wanapokaa na kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu ambaye pia hutambulishwa kama Mwokozi wao, kuzaliwa kwake kunaambatana na mambo mawili ambayo ni kuwa mtawala, kama unabii wa utabiri wa kuzaliwa kwake unavyozungumza.

Askofu Lwiza amesema. kuwa jambo la pili lililoambatana na kuzaliwa kwa Yesu ni kuwa mchungaji atakayewachunga watu wa Mungu na kama ambavyo naye alijitambulisha kuwa ndiye mchungaji mwema.

Akifafanua mamlaka hayo aliyopewa Yesu, Askofu Lwiza amesema kuwa ni mamlaka dhidi ya nguvu za giza, shetani na kifo na kwamba uchungaji wake ni kiwafundisha watu neno la Mungu na kuwafariji.