Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Kilaini aeleza alivyofurahi kuyaona maandamano ya Chadema

Muktasari:

  • Askofu Methodius Kilaini amesema Serikali inapaswa iuvumilie upinzani na vivyo hivyo upinzani uivumilie Serikali, pande zote ziichokozane na kuleta shida.

Dar es Salaam. 2024, Huku akihimiza kuvumiliana, Askofu Methodius Kilaini amesema alifurahi kuona maandamano ya Chadema yameruhusiwa na kufanyika kwa amani, vinginevyo ingeleta shida.

Akizungumza na Mwananchi Digital kuhusu masuala mbalimbali, Askofu huyo ambaye amestaafu hivi karibuni, ameshauri zitengenezwe sheria nzuri zaidi ya zilizopita zitakazoweka usawa katika Taifa.

Askofu Kilaini ametoa ushauri huo, kufuatia mjadala wa miswada ya sheria ya uchaguzi ya vyama vya siasa unaohitimishwa bungeni Dodoma leo Februari 2, 2024, licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya maandamano makubwa kushinikiza iondolewe bungeni.

Miswada hiyo ni wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na nadiwani, wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, yote ya mwaka 2023.

Akielezea hisia zake baada ya Serikali kuruhusu maandamano ya Chadema Januari 24, 2024, Askofu huyo amesema alifurahi kuyaona.

Chama hicho cha upinzani kilifanya maandamano ya amani kuelekea Umoja wa Mataifa yakilenga kuitaka Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu haja ya kuondoa bungeni miswada ili kufanya kwanza marekebisho ya Katiba ya 1977.

Pia Chadema ilitaka Serikali itengeneze mpango wa dharura wa kukabiliana kwa kupanda gharama za maisha kwa Watanzania na mfumuko wa bei.

“Nilifurahi walipoyaruhusu (maandamano), wangeyapinga tungepigana marungu, jambo ambalo si jema,” alisema askofu huyo aliyewahi pia kuwa Askofu Msaidi wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam, kabla ya kuhamia Bukoba hadi kustaafu kwake.

Kilaini amesisitiza iwepo haki na amani kwenye uchaguzi, akisema kwamba huwezi kuwa na amani bila haki.

“Jambo la kwanza kwenye chaguzi zetu, kuwepo na haki, pili ni amani, halafu tuvumiliane, bila hivyo hatuwezi kwenda mbele.

“Serikali iuvumilie upinzani na vivyo hivyo kwa upinzani uivumilie Serikali. Wasichokozane, unapomchokoza mmoja, atarudisha, italeta shida.

“Twende vizuri kwa upendo utakapofika uchaguzi, kwa kuwa sote tunajenga nyumba moja Tanzania,” amesema.


Sheria nzuri

Kilaini aliyekuwa askofu msaidizi wa Jimbo la Bukoba kabla ya kustaafu hivi karibuni amesema hakuna nchi yenye sheria zilizokamilika kabisa, lakini zinarekebishika na kufanya vitu viende mbele.

Akitolea mfano nchi ya Italia, alisema, “niliishi huko,  (Italia) ilikuwa ina sheria za kidemokrasia sana, lakini Serikali yao ilikuwa ikianguka kila baada ya muda mfupi.

“Ninachoweza kushauri hapa kwetu, tunapaswa kuwa na sheria nzuri zaidi kuliko zilizopita, tunafahamu wanasiasa wote huwa wanataka kuingia madarakani na wale waliomo huwa hawataki kutoka.

“Nishauri tu, sheria tulizonazo zijaribu kuweka usawa, Italia walishindwa kujadili kitu kikapita, sababu hawakuwa na chama tawala.

Mara nyingi huwa hakuna demokrasia iliyokamilika kabisa, lakini tujaribu kwenda mbele kwa kuongeza hiki na kile na tunachokipata tukitumie.

Kitu kibaya ni kutoka, ukitoka maana yake haumo kwenye mfumo na mara zote hauwezi kuigeuza Serikali ukiwa nje,” amesema askofu huyo.

Askofu Kilaini ameyasema hayo wakati mwaka huu,Taifa likisubiri kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu hapo mwakani.