Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu: Charles Hillary mtu makini, alipenda kanisa

Muktasari:

  • Askofu Jackson Sostens wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam amesema Charles Hillary alikuwa mshirika mwaminifu, mpenda kanisa na mtu makini.

Dar es Salaam. Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Jackson Sosthenes amesema Charles Hillary. alikuwa mtu makini na alilipenda kanisa.

Kabla ya umauti, Charles alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Charles alifariki dunia Mei 11, 2025 wakati akipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila jijini Dar es Salaam.

Katika misa ya kumuaga mwanahabari hiyo huyo iliyofanyika leo Jumanne Mei 13, 2025 katika Kanisa la Anglikana Ubungo jijini Dar es Salaam, Askofu Sosthenes amesema:

“Umakini wake unathibitika pia kwa kuwa shabiki wa Simba kwa kufanya uchaguzi sahihi kwa muda wote wa maisha yake duniani hadi Mungu anamuita.

Kwa hiyo mimi mwana Simba mwenzake nazidi kuwapa pole wana Simba wenzetu kwa kuondokewa na mtu ambaye ni muhimu kwa namna moja au nyingine,” amesema. 

Amesema Charles amekuwa mshirika mwema ndani ya kanisa hilo na hata alipoteuliwa mtumishi serikalini alimshirikisha, naye alimtia moyo akibainisha kuwa taarifa ya kifo chake ilimchukua muda kuamini.

Amesema mchango wa Charles kanisani hapo ulikuwa mkubwa na ameacha pengo kwa umoja wa akina baba kanisani hapo, kwa namna ambavyo alihakikisha kazi ya Mungu wanaifanya kwa umoja.

Kwa upande wake Mshauri wa Kanisa la Anglikana Ubungo, Moses Manyatta emesema Charles alikuwa mtu wa kujitoa kanisani hapo na ndiye aliyefanikisha michango ya vifaa vya uanzishwaji wa runinga mtandao wa kanisa hiyo.

"Tulianza kujenga kanisa hili tangu 2009 na tumekuwa na Charles kwa muda mrefu, alikuwa mtu wa kujitoa sana hata akiwa Unguja bado aliendelea kutuma michango yake na alitoa wazo la kuanzishwa hii runinga, awe anashiriki ibada akiwa huko," amesema.


Maisha yake duniani

Mtoto wake, Faith Charles akisoma wasifu wa baba yake kanisani hapo, amesema baba yake ni mtoto wa pili wa Martin Hillary na alizaliwa Oktoba 22, 1959 katika mtaa wa Jangombe na kukulia Mahadara mjini Zanzibar.

Kwa makubaliano kati ya wazazi na ndugu zake, Charles alitakiwa kuhamia Dar es Salaam kwa ajili ya masomo, japo changamoto iliyojitokeza ni kukosa mtu wa kusafiri naye kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam.

Faith amesema baba yake akiwa na miaka tisa alihamia Dar es Salaam na mama yake mdogo, ambaye aliishi naye Ilala Mchikichini na baadaye Kijitonyama.

 "Alianzia Shule ya Msingi St Paul Kiungani Zanzibar 1966 hadi 1968 alipohama na baadaye kusoma Shule ya Msingi Mchikichini Dar es Salaam 1969-1975,

Pia alisoma masomo ya Sekondari Kinondoni Muslim 1976 hadi 1979 , “ amesema.

Kuhusu utangazaji, Faith amesema 1980 aliajiriwa na Radio Tanzania akifanyia kazi zake Barabara ya Pugu Dar es Salaam.

Akiwa ndani ya radio hiyo alipewa mafunzo mbalimbali na kuonyesha kipaji chake na alifanya kazi hadi 1994 na baadaye kujiunga na Radio One chini ya Kampuni ya IPP.

Faith amesema mwaka 2003 alijiunga na Shirika la DW la Ujerumani na kufanya kazi

hadi 2005 mkataba wake ulipotamatika na kurejea nchini, mwaka 2006 akajiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na mwaka 2015 mkataba wake uliisha.

Kutoka hapo alirejea na kujiunga na Azam TV na kufanya kazi hadi 2021 alipotteuliwa na Rais Mwinyi kuwa Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu.

Mtangazaji huyo ameacha mke na watoto wawili Faith na Josephine na mjukuu mmoja.

Akitoa salamu za rambirambi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema ni aibu kumuaga Charles katika kanisa alilosali nyakati zote na akaliacha bado linajengwa.

Hivyo, amewaomba waombolezaji kuacha alama kanisani hapo"

Baba Askofu kaniambia zinahitajika Sh50 milioni ili kuondoa nguzo nje, haiwezekani tukaingia humu ndani na kumtaja huyu baba bila kuacha sadaka kanisani," amesema.