Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu asema kifo cha pacha walioungana ni somo kwa Watanzania

Muktasari:

Asema kila mtu anatakiwa kukumbuka kuishi vyema na watu wenye ulemavu, kutowabagua kwa namna yoyote ile.

Iringa. Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya pacha walioungana,  Maria na Consolata Mwakikuti kinapaswa kuenziwa na Watanzania kukumbushana  wajibu wao kwa watu wenye ulemavu.

"Wameacha somo hilo, tuwajali watu wenye ulemavu hilo ndilo somo walilotuachia Maria na Cobsolata," amesema Akofu Maluma leo Jumatano Juni 6, 2018 katika ibada ya kuaga miili ya pacha hao.

Amesema Mungu aliwaumba pacha hao kwa mfano wa sura yake na akawapa uhai kwa kipindi walichokuwa duniani.

Amebainisha kuwa masista wa shirika la Maria Consolata wameonyesha mfano wa kuigwa kwa kuwaleta pacha hao waliofariki dunia katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.

“Ni wakati wa taasisi na mashirika mengine kuweka jitihada katika kuwajali walemavu,” amesemana kubainisha kuwa ipo jamii inayoendelea kuwatenda wenye ulemavu na kuona kama kundi lisolofaa.

"Tuishukuru pia Serikali, imetimiza wajibu wake kwa maisha ya Maria na Consolata. Katika mema mengi tuliyojaliwa kutekeleza wajibu wetu ni  kusimamua uhai wa mwingine. Serikali na wote tufanye hivi kwa nia njema,” amesema.