Asilimia 36 waliofariki mafuriko Hanang ni watoto

Baadhi ya askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji wa Mkoa wa Manyara, wakiwa juu ya paa za nyumba wakijaribu kuokoa watu kwenye maafa yaliyosababisha vifo 47 na majeruhi 85 kwenye kata za Gendabi na Katesh wilayani Hanang. Picha na Joseph Lyimo
Hanang. Mwananchi Digital imekuandalia mchoro wa takwimu (Infographic) kuhusu maafa ya maporomoko ya matope yaliyotokea wilayani Hanang mkoani Manyara, ambapo takwimu hizo ni kwa mujibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu hadi Desemba 5, 2023 saa 3.10 asubuhi.
Maporomoko hayo yalitokea usiku wa kuamkia Jumapili Desemba 3, 2023 kutokana na mvua iliyonyesha kusababisha sehemu ya Mlima Hanang kumomonyoka.