Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ashikiliwa kwa madai ya kujifanya mtumishi wa Serikali

Muktasari:

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia Gabriel Kaserikali (34) Mkazi wa Mbezi mwisho Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa Serikali.

  

Iringa. Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia Gabriel Kaserikali (34) Mkazi wa Mbezi mwisho Jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kujifanya mtumishi wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari, leo Alhamisi Oktoba 13, 2022 Kamanda wa Jeshi la mkoani humo, ACP Allan Bukumbi amesema tukio hilo limetokea Oktoba Mosi, 2022 katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iringa iliyopo kata ya kihesa Manispaa ya Iringa mkoani humo.

Aidha ACP Bukumbi amedai mtuhumiwa alijitambulisha kwa baadhi ya wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM, Wilayani Iringa kwamba yeye ni Afisa usalama wa Taifa kutoka Makao Makuu Dodoma huku akiwaeleza wajumbe hao wamchague ndugu yake aitwaye Leonard Mgina kwenye nafasi ya uenyekiti  Wilaya kwamba ni maelekezo kutoka mamlaka ya juu za Serikali.

Kamanda huyo amesema kuwa baada ya Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na kubaini kuwa mtuhumiwa huyo siyo mtumishi wa idara ya usalama wa Taifa lakini pia alifanikiwa kumtapeli mfanyabiashara wa magari wa Magomeni jijini Dar es Salaam.

"Tumefanya uchunguzi na kubaini kuwa mtuhumiwa huyo siyo mtumishi wa idara ya usalama wa Taifa kwa sababu amemtapeli Mohamed Nassoro mfanyabiashara wa magari wa magomeni jijini Dar es salaam baada ya kujitambulisha kuwa ni mtumishi kutoka Idara hiyo" amesema ACP Bukumbi

kamanda huyo amedai kuwa baada ya mtuhumiwa huyo kujitambulisha kuwa mtumishi wa idara hiyo  ndipo walifanya makubaliano ya malipo ya awamu ya  kiasi cha Sh18.5 milioni lakini hakuweza kulipa kiasi chochote na kisha kutoweka na gari hilo.

Hata hivyo, Mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo.