Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Apandishwa kizimbani kwa kunaswa akiuza bangi Mbagala

File Photo

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imempandisha kizimbani Andrew Mpazi (47) Kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 21.31.

By Brighton Samwel na Grace William

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imempandisha kizimbani Andrew Mpazi (47) kwa kosa la kufanya biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 21.31

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali Tumaini Maingu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio amedai kuwa Julai 30, 2023 maeneo ya Mbagala Rangi Tatu mshtakiwa alikutwa akifanya biashara ya  dawa za  kulevya yenye uzito wa gramu 21.31 kinyume na sheria.

"Maeneo ya Mbagala Rangi Tatu mshtakiwa alikutwa akifanya biashara ya dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gramu 21.31  na upelelezi wake umekamilika tunaomba mahakama tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali," alidai  Maingu.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo.

Hakimu Mrio amesema kutokana na uzito wa gramu hizo, kesi hiyo haina dhamana na mshatakiwa atakwenda mahabusu.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 14, 2023 itakapokuja kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali.