Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyepotea wiki moja akutwa ameuawa, Polisi yatoa kauli

Muktasari:

  • Familia ilieleza kuwa Sarai alichukuliwa na watu wanne, mmoja akifahamika anaishi mitaa ya karibu Mei 22 mwaka huu na hakuonekana tena hadi Mei 27, mwili wake ulipobainika umefukiwa shambani eneo la jirani.

Tanga. Mkazi wa Mtaa wa Pande Malembwe, jijini Tanga, Sarai Kagoro (30), ameuawa kwa kuchinjwa na mwili wake kukatwakatwa kisha kufukiwa shambani, baada ya kupotea kwa takribani wiki moja.

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo, huku wengine watatu wakiendelea kutafutwa.

Akisimulia tukio hilo, kaka wa marehemu na msemaji wa familia, Jumaa Twaha, ames-ema leo Ijumaa Mei 30, 2025, kuwa Sarai alichukuliwa na watu wanne waliokuwa wakizunguka naye mtaani siku aliyopotea, Alhamisi. Taarifa za kutokumuona zilitolewa na familia baada ya kutorejea nyumbani na simu zake kubaki ndani.

Familia ilitoa taarifa polisi siku ya Ijumaa, ambapo jalada la uchunguzi lilifunguliwa. Jumamosi, baadhi ya watu waliotajwa kuwa na marehemu walichukuliwa kwa mahojiano.

Ndugu na jamaa wa marehemu Sarai wakionyesha sehemu ambayo walikuta shimo ambalo alifukiwa baada ya kuuawa na watu wanaodaiwa kuwa ni marafiki zake na kugunduliwa na mwenye shamba. Picha na Rajabu Athumani

Jumaa amesema Jumanne Mei 27, walipig-iwa simu usiku na polisi kwenda eneo la Mabayani ambako kulionekana sehemu iliyochimbwa ardhini. Jumatano Mei 28, polisi walichimba eneo hilo na kubaini mwili wa Sarai akiwa amechinjwa na kukatwakatwa, huku ukiwa umeharibika.

Mwili ulifanyiwa uchunguzi shambani kwa kushirikiana na wataalamu wa afya na kuzikwa hapo hapo kwa makubaliano ya familia.

Marehemu Sarai Kagoro (30) ambaye ameuawa na kukatwa viungo vya mwili wake na kisha kufukiwa shabani baada ya kupotea takribani wiki moja enzi za uhai wake.

Baba mdogo wa marehemu, Kasrani Sele-mani, amesema tukio hilo linahusiana na utekaji na kuomba wahusika wote waka-matwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Maketi Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtu mmoja anashi-kiliwa, huku juhudi za kuwatafuta wengine zikiendelea.

Kamanda amesema waligundua sehemu ya mwili kufukiwa baada ya mwenye shamba kwenda kukagua na kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Sarai wakionyesha kaburi ambalo amezikwa ndugu yao baada ya kukabidhiwa mwili na jeshi la Polisi walipokamilisha uchunguzi. Picha na Rajabu Athumani



Diwani wa Kata ya Kiyomoni, Mohamedi Mfundo, amesema ni tukio la kwanza kutokea katika kata hiyo na limewaacha wananchi wengi na mshangao. Amesema wanafanya juhudi za kuanzisha kituo cha polisi kusaidia usalama wa eneo hilo.

Wananchi wametakiwa kuendelea ku-shirikiana na polisi ili kuwabaini wote wali-ohusika na tukio hilo la kikatili.