Mtoto adaiwa kuua wazazi wake Moshi

Muktasari:
- Tukio hilo lilitokea Mei 29, 2025 na mwili wa mwanaume huyo ulikutwa umekatwa shingoni na kitu chenye ncha kali, wa mwanamke haujakutwa na majeraha.
Moshi. Wanandoa Godfrey Mota (60) na Blan-dina Ngowi (53), wakazi wa Msufuni, Msaranga, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameuawa kikatili huku mtoto wao ambaye ametoweka, akishukiwa kuhusika.
Inaelezwa kuwa kijana huyo, ambaye anadaiwa kuwa na tatizo la afya ya akili, mara kwa mara alikuwa akiwatishia wazazi wake na kuwatamkia maneno kwamba ipo siku atawaua.
Inadaiwa kuwa siku ya tukio, kijana huyo aliku-wa nyumbani hapo anakata miti lakini baada ya tukio hilo hajaonekana tena mtaani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, ndani ya nyumba ya kupanga ambayo familia hiyo ilikuwa ikiishi Mei 29, 2025.
Kamanda Maigwa amesema mwili wa mwa-naume huyo umekutwa umekatwa shingoni kwa kitu chenye ncha kali, huku wa mwanamke uki-wa hauna majeraha ya nje.
"Tukio hilo limetokea ndani ya nyumba wali-yokuwa wakiishi wanandoa hao pamoja na kija-na wao wa kiume ambaye ametoweka baada ya mauaji hayo kutokea," amesema Kamanda Maigwa.
Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha mauaji hayo, na kwamba yeyote atakayebainika kuhusika atachukuliwa hatua za kisheria. Miili ya marehemu imehifad-hiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa uchunguzi zaidi.
Watoto wasimulia
Haika Godfrey, mtoto mwingine wa marehemu, amesema siku ya tukio alijaribu kupiga simu za wazazi wake bila mafanikio; moja ilikuwa inaita bila kupokewa na nyingine ilikuwa haipatikani kabisa hewani.
Amesema hali hiyo ilimpa wasiwasi mkubwa kwa kuwa alikuwa na mazoea ya kuwasiliana na wazazi wake mara kwa mara kujua hali yao.
Haika amesema kufuatia wasiwasi huo alimtuma kaka yake, ambaye alikuwa akitokea Arusha, kwenda kuwajulia hali wazazi wao, kwa kuwa yeye siku hiyo alimpeleka mtoto wake hospitali.
"Ilipofika saa 12 kasoro jioni nilifika nyumbani kwa mama, maana simu zao zilikuwa hazi-patikani. Nilipoingia ndani moja kwa moja, ni-kakuta mwili wa mama chini akiwa amelalia da-mu iliyoganda. Wakati huo, kwa kuwa nilichang-anyikiwa, sikuona mwili wa baba kitandani. Ni-lidondoka chini na kusaidiwa na mtu aliyenileta kutoka hospitali," amesimulia Haika.
Amesema baada ya kuzinduka alipiga simu kwa viongozi wa eneo hilo ambao walimsaidia ku-wasiliana na polisi. Askari walifika na kuchukua miili ya marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Mtoto mwingine wa marehemu, Abraham God-frey, amesema tukio hilo ni pigo kubwa kwa fa-milia yao na ni kumbukumbu mbaya ambayo haitafutika.
"Tukio hili linaumiza kwa kuwa hakuna mtu anayetegemea kupoteza wazazi wake wote kwa wakati mmoja. Hata mmoja tu akifa ni uchungu, sembuse wote. Kila mtoto hupenda ajitume afanye kazi ili baadaye awarudishie wazazi wake kwa shukrani," amesema Abraham.
"Wazazi wangu wameuawa kwa kushambuliwa na silaha. Baba alipigwa kichwani na kukatwa shingo pamoja na katikati ya kichwa, na mama ni kama alinyongwa. Kupoteza wazazi wangu wote ni pigo kubwa, nimeumia sana."
Amesema hadi sasa mdogo wao ambaye aliku-wa akiishi na wazazi hajulikani alipo tangu kutokea kwa tukio hilo.
"Huyu mdogo wetu tangu mwaka 2022 alikuwa kama amechanganyikiwa. Baadaye wa-lishughulikia tatizo hilo na likapungua, lakini baada ya miezi 10 tatizo likarudi. Ikawa kazi yake ni kuzunguka tu. Sasa baada ya tukio hili, hajaonekana kabisa," amesema Abraham.
Kauli ya Kanisa
Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Msaranga Mandaka wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanza-nia (KKKT), Samson Lazier amelaani vikali tukio hilo na kuwataka watu kuthamini uhai wa wen-zao.
"Wanausharika wetu wamechinjwa na mpaka sasa hajajulikana ni nani hasa aliyefanya hivyo. Tukio hili ni la kuchukiza sana. Mungu hataki na amekataza katika amri zake kwamba usiue," amesema Mchungaji Lazier.
"Tunaendelea kukemea mauaji haya katika ja-mii, ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu na kinyume na sheria ya nchi yetu, kwamba kuua mtu ni kosa kisheria."
Ameviomba vyombo vya dola kuchunguza suala hilo kwa kina na kuhakikisha waliohusika wana-chukuliwa hatua kali.
"Tunaomba vyombo vya usalama vichukue hatua madhubuti katika kulinda amani na kuzuia ukatili. Tukio hili tunalikemea kwa nguvu zote," amesema Mchungaji Lazier.