Aliyemtapeli mpangaji NHC apandishwa kizimbani Dar

Muktasari:
- Anayedaiwa kujipatia Sh3 milioni ili asimtoe mpangaji kwenye 'Apartment', apandishwa kizimbani Dar
Dar es Salaam. Ofisa Miliki, Fadhil Kasegese amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka mawili ambayo ni kuomba rushwa ya Sh4 milioni na kupokea rushwa ya Sh3 milioni.
Kasegese anadaiwa kujipatia fedha hiyo kutoka kwa Vishal Dharsi ili asimtoe kwenye ' Apartment ' aliyokuwa amepanga iliyopo Mtaa wa Msimbazi Kariakoo, inayomilikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka leo, na wakili wa Serikali Mwandamizi Mwanakombo Rajabu akisaidiana na Henry Mahengo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Ramadhani Rugemarila.
Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 3, 2023 na Aprili 6, 2023 katika ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Ilala jijini hapa.
Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabili amekana kutenda na yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Kwa habari hii na nyingine nyingi, endelea kufuatikia mitandano yetu ya kijamii.