Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyehukumiwa miaka 20 kwa kukutwa bangi, aachiwa

Muktasari:

  • Alikata rufaa akiwa hoja saba, ikiwemo upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha kosa hilo.

Arusha. Mahakama Kuu Masijala ndogo ya Mtwara, imemuachia huru Kangomba Mohamed, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 49.64.

Mahakama hiyo imemuachia huru baada  ya kubaini dosari za kisheria wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama ya chini.

Baada ya kupitia mwenendo wa shauri la jinai namba 12/2023 lililosikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tandahimba, Mahakama Kuu ilitengua adhabu hiyo na kuamuru aachiwe.

Rufaa hiyo ya jinai namba 11259/2024, ilisikilizwa na kutolewa uamuzi na Jaji Martha Mpaze, Julai 18, 2024.

Ilidaiwa usiku wa Januari 25, 2023 shahidi wa kwanza, Inspekta Tito Kingwile, akiwa na askari wenzake tisa kwenye doria katika Kijiji cha Chingungwe, walimkuta mrufani akiendesha pikipiki yenye namba za usajili MC 344 CTD, huku akiwa amebeba magunia manne na kumsimamisha.

Alidai baada ya kusimama walipekua ndani ya magunia hayo na kukuta dawa hizo za kulevya na kumuweka chini ya ulinzi,  kisha kumpeleka kituo cha Polisi Tandahimba.

Mrufani alishtakiwa kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya dawa kinyume na Kifungu cha 15A(1) na (2)(b) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, namba 19 ya mwaka 2019.

Mrufani huyo alidaiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya zenye uzito wa kilo 49.64 kutoka Masasi hadi Mtwara Mjini.

Mahakama ya chini, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi wanne, huku mrufani akijitetea mwenyewe, ambapo baada ya Mahakama kusikiliza ushahidi wa pande zote iliridhika upande wa mashtaka umethibitisha shtaka dhidi ya na kumhukumu adhabu hiyo.


Rufaa

Mrufani huyo alikuwa na sababu saba za rufaa, ikiwemo upande wa mashtaka kutothibitisha kesi yake bila shaka yoyote, mlolongo wa ulinzi (wa dawa zilizokamatwa haukuhifadhiwa) na hakuna maelezo kutoka kwa shahidi wa tatu juu ya hilo.

Sababu nyingine ni kielelezo cha saba ambacho ni ripoti ya mchambuzi wa Serikali ilitolewa kwa njia isiyofaa na shahidi asiye na uwezo, hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alijielekeza vibaya kwa maelezo ya onyo na maelezo ya ziada ya Mahakama hayakuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Hoja nyingine ni Mahakama ilishindwa kuchunguza, kutathmini na kuchambua ushahidi kwenye kumbukumbu na Mahakama Kuu kubatilisha na kutengua adhabu aliyopewa.

Katika usikilizwaji wa rufaa hiyo, mrufani alijiwakilisha mwenyewe huku mjibu rufaa akiwakilishwa na Wakili Florence Mbamba.

Katika hoja ya rufaa hiyo, mrufani aliitaka Mahakama kuzingatia sababu za rufaa yake kama ilivyowasilishwa, akisisitiza kutokuwepo kwa shahidi muhimu ambaye ni Mkemia wa Serikali haiwezi kusemwa kuwa kesi hiyo ilithibitishwa pasipo shaka.

Kwa upande wake, mjibu rufaa aliunga mkono rufaa hiyo kwa misingi kadhaa ikiwemo hoja ya pili, tatu na akieleza ni kweli utaratibu wa upokeaji wa vielelezo hivyo ni pamoja na mlolongo wa ulinzi, hati ya ukamataji na taarifa ya tahadhari, haikufuatwa.

Wakili alieleza kabla ya vielelezo hivyo kupokelewa, hakuna msingi uliowekwa, wala haukutambuliwa au kuondolewa kabla na kuwa vilisomwa kwanza kabla ya kupokelewa.

Wakili huyo aliongeza kuwa magunia manne yanayoshukiwa yana bangi, ripoti ya mchambuzi wa serikali, fomu ya kuwasilisha na barua ya kuomba uchambuzi ufanyike, pia zilikubaliwa bila kufuata utaratibu unaofaa.

Aidha, kielelezo pekee ambacho wakili huyo wa Serikali alisema kilikubaliwa kwa mujibu wa utaratibu ni taarifa ya ziada ya Mahakama na kukubali upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha kesi hiyo bila kuacha shaka.

Aliongeza kuwa Mkemia wa Serikali, shahidi muhimu katika kesi kama hizo, hakufika kortini kuthibitisha ikiwa majani hayo yaliyokuwepo kwenye magunia yalikuwa ni bangi.

Kutokana na kasoro hizo, wakili huyo alisisitiza katika mazingira hayo, haiwezi kusemwa kuwa upande wa mashtaka ulithibitisha kesi yao bila kuacha shaka.


Hukumu

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Martha alieleza hoja ya kuwa ikiwa shtaka limethibitishwa bila shaka yoyote kunahitaji kuchunguza ushahidi unaotolewa mahakamani, iwe ni wa mdomo, hali halisi au ushahidi halisi.

Alieleza katika mazingira hayo, haiwezi kuepukika kuunganisha ushahidi wa mdomo uliotolewa na vielelezo vilivyotolewa, ili kuona kama shtaka lilithibitishwa bila shaka yoyote, huku akinukuu kesi ya Mahakama ya Rufani.

Jaji alieleza kwa kuongozwa na kile kilichosisitizwa katika kesi tajwa, mrufani analalamikia vielelezo hivyo vilipokelewa mahakamani bila kufuata utaratibu, ikiwemo cheti cha kukamata na maelezo ya onyo.

Jaji alieleza vielelezo vyote vimepokelewa bila kuwekewa msingi wowote ni msimamo wa kisheria kwamba kabla ya kielelezo kuwasilishwa na kupokelewa mahakamani, ili kuwa sehemu ya ushahidi, shahidi anayetaka kukitoa lazima aweke msingi kabla hakijakubaliwa.

Huku akinukuu mashauri mbalimbali yaliyotolewa maelezo na mahakama ya rufani, alieleza kuanzia ushahidi wa shahidi wa kwanza mbali na kutoa cheti cha ukamataji, alitoa magunia yaliyoshukiwa kuwa na bangi na katika ushahidi wake alipotoa kielelezo hakuweka msingi wowote.

“Wala hakueleza ni vitu gani vitaonekana kwenye cheti alichokamata siku alipojaza cheti hicho cha ukamataji na nani alishuhudia na kusaini cheti hicho cha ukamataji,” alieleza Jaji.

“Si hivyo tu shahidi wa kwanza  alishindwa kueleza iwapo wakati wa kukamatwa na kujaza cheti cha ukamataji, kulikuwa na shahidi yeyote wa kujitegemea ambaye alishuhudia kukamatwa na kusaini hati ya ukamataji, wala hakueleza iwapo mshtakiwa pia alisaini,” aliongeza.

Jaji Martha alieleza kwa kanuni za kisheria zilizowekwa, kusainiwa kwa cheti cha kukamata ni muhimu, kwani inathibitisha mali hiyo ilichukuliwa kutoka kwa mshtakiwa.

“Kushindwa kuweka wazi ukweli huu kabla ya kukubali vielelezo katika ushahidi kunaweza kuzua shaka iwapo magunia yanayodaiwa yalipatikana katika milki mshtakiwa, hakuna msingi uliowekwa, vielelezo havikufutwa au kutambuliwa kabla ya kutolewa na kukubaliwa,” aliongeza

Jaji alieleza shahidi wa kwanza hakueleza alihifadhi wapi magunia hayo baada ya kumkamata mrufani na kuwa alitarajia kwa vile yeye ndiye aliyempeleka mrufani kituo cha polisi akiwa na magunia hayo, angeeleza alama alizoweka wakati wa makabidhiano ya magunia.

Alieleza ushahidi wa shahidi wa pili ni kuhusu kuchukua maelezo ya onyo ya mrufani, huku shahidi wa tatu akieleza kuhusu kupeleka magunia manne ya bangi kwa Mkemia wa Serikali kisha kupeleka kwa mtu mwingine ambaye hakufika mahakamani kutoa ushahidi wake.

Jaji alieleza ni wazi kwamba utaratibu haukufuatwa wakati vielelezo hivyo vinatolewa mahakamani na hivyo kuna dosari ilivyofanya vielelezo kuanzia cha kwanza hadi cha 10 kuondolewa kwenye rekodi.

“Baada ya vielelezo hivi kufutwa kwenye kumbukumbu, hasa kielelezo cha kwanza ambayo ndiyo msingi wa shtaka hili, hata kama ningeendelea kubaini suala la iwapo Mahakama ya awali ilichunguza, kuchambua na kutathmini ushahidi huo, itakuwa ni kazi bure, kwani ushahidi uliobaki hauwezi kuthibitisha vya kutosha hatia ya mrufani,” alihitimisha.