Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alberto Msando ajiuzulu nafasi ya ushauri ACT

Wakili Alberto Msando

Muktasari:

  • Uamuzi huo umekuja zikiwa zimepita siku chache tangu  kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii video ikimwonyesha akifanya vitendo visivyo na maadili.

Dar es Salaam. Wakili Alberto Msando amejiuzulu nafasi yake ya ushauri wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne na kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe imeeleza kuwa Msando ameandika barua ya kujivua wadhfa huo ambayo imepokelewa na chama hicho.

“Ndugu Msando anawajibika kwani anapaswa, nanukuu  ‘kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka.’Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama,”amesema Zitto.

Zitto amesema Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya ACT.

“Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake. Msando ameomba msamaha kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba,”amesema Zitto.