Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali ya basi yaua 11, yajeruhi 44 Mbeya

Basi la Kampuni ya A-N Coach baada ya kupata ajali katika eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini leo Septemba 6, 2024.

Muktasari:

  • Ajali hiyo imetokea kutokea leo alfajiri katika eneo la Luanjilo, Wilaya ya Mbeya baada ya basi la A-N lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka.

Mbeya. Watu 11 wamepoteza maisha na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya A-N Coach kupata ajali katika eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Ijumaa, Septemba 6, 2024 baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka wakati likilikwepa lori, kisha kutumbukia mtaroni.

Mganga wa Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Chunya, Dk Darson Andrew amethibitisha kupokea idadi ya hiyo na vifo huku akieleza kati ya majeruhi 44 wanne wana hali mbaya na watapewa rufaa kupelekwa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Kamanda msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, Wilbert Siwa amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba yuko eneo la tukio akishughulika kuhakikisha majeruhi kuwapeleka hospitali.

“Ni kweli ajali imetokea na nipo eneo la tukio, naomba nimalize kushughulikia hawa majeruhi waende hospitali kisha nitaelezea zaidi,” amesema Siwa.


Endelea kufuatia Mwananchi