Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ADC ‘yavuna’ 280 kutoka CCM, Chadema na ACT-Wazalendo

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Shaaban Itutu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea wanachama wapya 280 walijunga na chama hicho wakitokea vyama vingine vya siasa. Picha na Anania Kajuni

Muktasari:

Wakati CCM imepoteza wanachama wake 120 waliotimikia ADC, Chadema imeondokewa na wanachama 50 huku ACT- Wazalendo ikipowapoteza wanachama 80 na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma) kimepoteza wanachama 30.

Mwanza. Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) imevuna wanachama wapya 280 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demorasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo.

Wanachama wapya hao wamepokelewa na Makamu Mwenyekiti wa ADC, Shaaban Itutu wakati wa hafla iliyofanyika Kata ya Isamilo jijini Mwanza Oktoba 15, 2023.

Wakati CCM imepoteza wanachama wake 120 waliotimikia ADC, Chadema yenyewe wameondokewa na wanachama 50 huku ACT- Wazalendo ikipowapoteza wanachama 80 na Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma) kikipoteza wanachama 30.

Melyina Aloce, mkazi wa Nyakabungo C jijini Mwanza aliyehamia ADC akitokea CCM ametaja kuvutiwa na sera, fursa ya kushiriki shughuli za kiuongozi na ahadi ya kushughulikia matatizo ya wananchi likiwemo suala la haki wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo kuwa baadhi ya sababu ya kujiunga na chama hicho.

‘’Naamini ADC ikishinda uchaguzi na kuongoza dola itashughulikia na kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi likiwemo hili la mgawo wa umeme unaokwamisha shughuli za kiuchumi,’’ amesema Melyina

Elias Kibutu, mwanachama mpya wa ADC aliyetokea CCM amesema kilichomfanya kukihama chama hicho tawala kwenda chama kingine ni kutafuta jukwaa la kushiriki kutatua matatizo ya wananchi akidai CCM imeishiwa mbinu na ubunifu kutokana na kukaa madarakani kipindi kirefu.

‘’Mfano hai ni huu mgawo wa umeme ambao umegeuka kuwa tatizo sugu licha ya Tanzania kujaaliwa kuwa na vyanzo vingi vya umeme kuanzia maji, joto ardhi, upepo, gesi na makaa ya mawe. Tatizo hapa ni chama kilichopo madaraka na viongozi wake kukosa fukra na mbinu mpya,’’ amesema Kibutu

Anasema uhakika wa huduma ya umeme wa wakati wa uongozi wa Hayati John Magufuli ni ushahidi kwamba tatizo la mgawo wa umeme linatokana na uongozi.

Mwanachama mpya wa ADC aliyehamia chama hicho akitokea ACT-Wazalendo, Angelina Sandarya yeye ametaja kuvutiwa na sera, uongozi shirikishi na kila mwanachama kupewa nafasi katika maamuzi ya chama kuwa miongoni mwa vilivyomvutia kuhamia chama hicho.

Akizungumza na wanachama wapya, Makamu Mwenyekiti wa ADC, Shaaban Itutu amesema kujitangaza kupitia shughuli mbalimbali za kisiasa, kusikiliza na kutatua matatizo ya wananchi na kupokea wanachama wapya ni miongoni mwa mbinu na mikakati ya chama hicho kuendelea kujiimarisha katika ulingo wa siasa kufikia lengo la kushinda uchaguzi na kuongoza dola.

"Ni wakati wenu ninyi wanachama wapya kushirikiana na mliowakuta na viongozi kukijenga chama chenu kwa kufanya shughuli za kisiasa katika maeneo yenu na kwa nafasi zenu ili hatimaye tufikie lengo la kushinda uchaguzi na kuongoza dola,’’ amesema Itutu