Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ACT yataka NHIF ifungamanishwe na hifadhi za jamii

Muktasari:

  • ACT-Wazalendo imependekeza masuala Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ufungamanishwe na hifadhi ya jamii ili kuleta ufanisi.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kivuli wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu amesema chama hicho kinapendekeza kufanyika maboresho ya mfumo katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kuleta ufanisi.

Akizungumza leo Aprili 10 wakati wa uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali uliofanywa na chama hicho jijini hapa, Semu amesema mwenendo wa sasa wa NHIF hauridhishi ikiwemo kutoa huduma kwa wanufaika ambao hawana wachangiaji.

Katika maelezo yake, Semu amedai NHIF inakufa kwa sababu mfumo wake sio endelevu na haulengi kuifanya taasisi hiyo kupata mapato yatakayowahudumia watu wengi.

“Ukaguzi wa CAG amebaini uwepo wa kadi hai za NHIF 21,042 ilizotumika kupokea huduma mbalimbali za afya na kutumia Sh 1.78 bilioni, lakini wamiliki wake hawakutoa mchango wowote,”amesema Semu.

Semu ameeleza hayo leo Jumatatu Aprili 10,2023 wakati akiwasilisha taarifa ya uchambuzi wa ripoti wa CAG iliyojikita katika maeneo 10 ikiwemo hali ya mwenendo wa utoaji huduma ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Mwezi uliopita akiwasilisha ripoti yake Ikulu Dar es Salaam, CAG Charles Kichere amesema ukaguzi wake ndani ya NHIF umebaini kuwa matumizi kutoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya yamekuwa makubwa ikilinganishwa na michango yao.

Kwa mujibu wa CAG Kichere, katika mwaka 2021/2022 mfuko umepata hasara ya Sh189.65 bilioni ikilinganishwa na Sh93.6 bilioni iliyokuwapo mwaka uliotangulia.

Lakini leo Semu amesema ili kuleta ufanisi wa NHIF, Semu chama hicho kinapendekeza suala la bima ya afya lifungamanishwe na hifadhi ya jamii. Kutokana na hilo wamependekeza mifumo ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PSSSF iwe na fao la matibabu litakalorahisisha mchakato huo na kuleta ufanisi.

Mbali na hilo, Serikali itoe vivutio kwa watu wasiokuwa sekta rasmi wakiwemo wafanyabiashara wadogo na mamalishe ili kujiunga na skimu ya hifadhi ya jamii kwa kuwchangia theluthi moja kila mwezi (Sh 10,000).

“Kwa pendekezo hili takribani watu milioni 7 watakuwa wanachama wa NHIF na mapato yataongezeka ya mfuko huu. Pia Serikali iwalipie kwa asilimia 100 wale wanufaika wa Tasaf (Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Tasaf) katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili moja kwa moja wawe wanachama wa NHIF,” amesema.