Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

15 Mbaroni tuhuma za wizi wa miundombinu ya barabara

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora SACP Richard Abwao akitoa taarifa ya wizi wa miundombinu ya taa za barabara katika wilaya ya Sikonge.Picha na Hawa Kimwaga

Muktasari:

  • Kumekuwa na wimbi la wizi wa miundombinu ya barabara kwa baadhi ya maeneo mkoani Tabora hali inayosababisha Jeshi la Polisi kufanya operesheni za mara kwa mara ili kukomesha vitendo hivyo.

Tabora: Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za wizi wa taa za barabarani, sola paneli na betri za sola  katika barabara ya Tabora kwenda mkoani Katavi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 29,2025 Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Tabora,  Richard Abwao amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako mkali uliofanywa mkoani humo kwa kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka huu.


Amesema upelelezi na mahojiano yanaendelea ili kubaini mtandao mzima unaohusika na wizi wa miundombinu ya barabara.

“Lazima tuwabaini watu wote wanaohusika na vitendo hivi na tutawakamata lazima na kuwafikisha mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake, lakini niwaase watu wachache wasio waaminifu kuacha tabia hizo kwani sheria haitawavumilia,”amesema  
Meneja wa Wakala ya Barabara (Tanroads), mkoani Tabora,  mhandisi Raphael Mlimaji amesema miundombinu iliyoibiwa imegharimu Sh80 milioni.


New Content Item (1)
New Content Item (1)

Amesema mbali na hasara hiyo kwa Serikali wizi huo  umesababisha adha kwa wananchi wa wilaya ya Sikonge kwani eneo hilo kwa sasa kuna giza kwa baadhi ya maeneo.

Akizungumzia hilo Mkuu wa Wilaya ya Sikonge,  Cornel Magembe amesema Serikali haitamvumilia yeyote anayehujumu miundombinu hiyo, huku akitoa onyo kali kwa wale wote wanaojaribu kuharibu au kuiba na kuitia hasara Serikali.

“Tumeshatangaza vita kwa wote wanaoshiriki vitendo hivi viovu haiwezekani watu wachache watusumbue hapa” amesema Magembe.

Rehema Abilahi mkazi wa Sikonge  amesema wamesikitishwa sana na wizi wa taa hizo kwani zimekua zikiwanufaisha hasa katika kukuza uchumi.

“Tulikua tunafanya biashara mpaka usiku kwa sababu taa zina mwanga mkali tunapata fedha tunahudumia familia zetu, lakini sasa hivi giza likiingia tu tunarudi nyumbani,”amesema.

Barabara hiyo ilizinduliwa Mei 18, 2022 na Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa imekamilika pamoja na miundombinu ya taa hizo.