Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi waandamana, wapinga kulipa Sh150,000 ya mitihani

Muktasari:

Wanafunzi hao walifika hadi kwa mkuu wa mkoa kulalamikia malipo hayo.

Mwanza. Wanafunzi zaidi ya 200 wa kidato cha sita katika shule ya Sekondari Taqwa ya jijini Mwanza wameandamana hadi ofisini kwa Mkuu wa mkoa huo kupinga kutozwa Sh150,000 kwa ajili ya ada ya mitihani ya majaribio na makaratasi.

Baada ya kuyapokea maandamano hayo, Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, Joseph Ngoseki amewataka wanafunzi hao kurejea shuleni akiahidi kufika kuwasikiliza mbele ya walimu na uongozi wa shule.

Akizungumza shuleni hapo, Ofisa Elimu huyo ameagiza wanafunzi wote kurejeshewa Sh30,000 kati ya Sh50, 000 walizotozwa kwa ajili ya mitahani ya majaribio ya kitaifa kwa sababu ada halali ni Sh20, 000 pekee.

“Ada kwa ajili ya mitihani ya majaribio ya Serikali ni Sh20,000 kwa wanafunzi wote bila kujali shule za umma wala binafsi kwanini shule hii imewatoza wanafunzi Sh50,000? Rejesheni Sh30,000 za ziada mlizotoza,” ameagiza Ngoseki.

Kuhusu kiasi kingine cha Sh100, 000 kilichosalia, ofisa elimu huyo ameuagiza uongozi wa shule kuandaa mchanganuo wake na kuuwasilisha ofisini kwake kwa uamuzi zaidi.

Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanafunzi Liliani Yusuph na Hamisi Hamisi wamemweleza ofisa elimu huyo kuwa juhudi zao za kuhoji uhalali wa malipo hayo zimeshindikana ndio maana wamefikia uamuzi wa kuandamana kuomba msaada ofisini kwa mkuu wa mkoa.

Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Muksini Rajabu ameahidi kuwa uongozi wake utatekeleza maelekezo yote ya ofisa elimu na kuwasihi wanafunzi hao kuendelea na masomo kujiandaa na mitihani ya majaribio na kitaifa baadaye mwezi Mei wakati suala hilo likitafutiwa ufumbuzi.