Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Ujumbe wa Askofu Shoo kwa Rais Samia mkataba wa bandari

Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo.

Dar es Salaam. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo amesema kuwa kanisa hilo linaunga mkono uwekezaji wa kampuni ya DP World katika bandari za Tanzania, lakini akatahadharisha suala hilo lisije likawagawa wananchi kwa misingi ya kidini kutokana na maoni tofauti yaliyoibuka.

 Askofu Shoo ameyasema hayo leo Agosti 21 katika maadhimisho ya miaka 60 ya kanisa hilo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Makumira, mkoani Arusha.

“Najua watu wengi wanasubiri Mzee Shoo atasema nini leo, lipo hili la DP World kwanza naomba ieleweke wazi kwamba kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingi uwekezaji Rais na tunajua wewe kwenye nia yako unataka wawekezaji.

 “Hata hivyo jambo hili limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi, vyombo vya habari, viongozi wa dini, lakini tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni kabisa mwa jambo hili.

Ujumbe wa Askofu Shoo kwa Rais Samia mkataba wa bandari

“Kwa uungwana wako na unyenyekevu na utayari wa kusikiliza ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama taasisi na viongozi wakuu wa dini, madhehebu yote, tukiwa CCT, TEC na Bakwata mimi nakumbuka jinsi ulivyotupokea.

“Ukatusikiliza ukapokea maoni yetu na ushauri yetu na ukaahidi maoni na ushauri huo utaupeleka kwa wataalamu na kuyafanyia kazi kwa uzito na maslahi mapana ya taifa.

“Tunakuamini na tunaamini kwamba ukisema taasisi zako na vyombo vyako vitafanyia kazi jambo hili, tunamaanisha jambo hilo.

“Sasa najua katika jambo hili tunaelekea mahali ambapo tunakaribia kugawanyika kabisa, wengine wanatumia sababu za kidini wengine wana maslahi yao ya kisiasa na maslahi ya kiuchumi.

“Nashukuru Mungu amekujaalia hekima kama mama na kiongozi umekaa kimya lakini kimya chako hicho sio kwamba hufanyii kazi, mimi nasema jambo hili linahitaji hekima kubwa ya kuliendelea na sisi tunakuombea kwa Mungu ili heshima yote itumike ili kuliendea jambo hili ili muafaka upatikane.

“Mheshimiwa Rais kanisa lipo pamoja na wewe, tutaendelea kukuombea na kukuunga mkono katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya nchi kwa maslahi mapana ya nchi.

“Umeweka wazi msimamo wako na tumeona watu wakiwa huru kueleza maoni yao na matumaini yetu iwapo watendaji wote wataielewa nia yako vema basi nchi yetu itadumisha amani na utulivu,” amesema

Kauli ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo katika maadhimisho ya miaka 60 ya kanisa hilo, jijini Arusha.