Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

'Tunzeni miundombonu usafi wakati wa hedhi'

Muktasari:

  • Kila Mei 28, duniani kote wadau wa afya na jinsia huadhimisha siku ya hedhi, huku ikiripotiwa kwamba asilimia 34 ya wasichana hukosa vipindi shule kutokana na upungufu wa vyumba maalumu vya kujisitiri wakati wa hedhi na asilimia 26 hukosa maji na vyoo safi wakiwa shule.

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiadhimisha siku ya hedhi, wito umetolewa kwa wananchi kulinda miundombonu ya usafi ikiwemo ya maji na vyoo vya shule ili kiwawezesha wasichana kuhudhuria masomo.

 Hayo yamesemwa leo Mei 28 na mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Handeni, Upendo Magashi baada ya kupokea miundombinu iliyokarabatiwa na vifaa vya usafi kutoka kwa shirikaa Water Aid kwa shule ya sekondari ya Misima iliyoko halmashauri ya mji wa Handeni mkoani Tanga.

Mbali na miundombinu, wanafunzi na walimu wamepewa mafunzo tabia siha uliofadhiliwa na shirika la Hilton Global Foundation pamoja na WaterAid ili kupunguza makali ya ukosefu wa maji katika shule hiyo hasa kwa watoto wa kike wanapokua katika kipindi cha hedhi.

“Miundombinu hii inahitaji kutunzwa ili iweze kutoa huduma husika kwa kipindi kirefu kwa sasa na kwa wanafunzi watakaokuja kusoma katika shule hii hivyo haina budi itunzwe,” amesema Magashi.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugezi wa Shirika la WaterAid Tanzania, Anna Mzinga amesema wamefanikisha ukarabati wa miundombinu ya  mfumo wa maji, matenki la kuhifadhia maji, vyoo ikiwemo kuweka muundombinu wa choo rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu .

"Pia tumetoa elimu kuhusu usafi kwa wasichana na wavulana  katika hatua za makuzi yao binafsi  hii ilijumuisha  mafunzo maalumu ya  namna ya kujitengezea  taulo za kike za kujisitiri wakati wa  hedhi ili kujilinda na adha mbalimbali  wanapokua katika kipindi cha hedhi," amesema.

Katika hafla hiyo Anna Mzinga amemkabidhi mkuu wa shule cherehani moja kwa ajili ya wanafunzi kujishonea pedi za kitambaa, vifaa 40 vya kushonea pedi, katoni 55 za pedi (kutumika katika kipindi cha mvua pale pedi za kufua zitashindwa kukauka).

Pia amekabidhi vifaa vya michezo seti 3, mabango 20 kwa ajili ya kujifunza masuala ya usafi na televisheni kwa ajili ya kujifunza tabia siha na usafi kwa ujumla.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Hedhi ni tunu na Msingi wa Afya kwa wasichana na Wanawake, Tuiwezeshe.”