Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali: Watanzania 210 waliopo Sudan wapo salama

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax

Muktasari:

Serikali imesema hakuna Mtanzania aliyezurika katika mapigano yanayoendelea nchini Sudani.


Dodoma. Serikali imesema hakuna Mtanzania aliyedhurika katika mapigano yanayoendelea nchini Sudani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax ameliambia Bunge leo Jumatano April 19, 2023 wakati akitoa kauli ya Serikali kuhusu mapigano nchini Sudan.

Mapigano yalizuka mwishoni mwa wiki iliyopita nchini humo na hadi leo Dk Tax amesema yameshasababisha vifo vya watu 185 na majeruhi zaidi ya 1000 ingawa kwa sasa yamesimama kwa muda wa saa 24.

Chanzo cha mapigano hayo ambayo yalianzia mji mkuu wa Khartoum, ni vikosi vya jeshi chini ya utawala wa Jenerali Abdul Fattah al-Burhan ambaye sasa ni Rais na wanachama wa kikosi cha kijeshi cha Rapid Support Forces (RSF).

“Mapigano hayo yamerudisha nyuma jitihada zinazoendelea kutafuta amani, Tanzania inaunga mkono tamko la Baraza la Amani la Umoja wa Afrika kwenye lililotolewa kwenye mkutano wa April 16, 2023 na inalaani mapigano hayo ikitaka pande mbili zinazofadhiana kusitisha mapigano,” amesema Dk Tax.

Waziri amesema Serikali inafanya mawasiliano ya mara kwa mara na ubalozi wake ili kujua hali za Watanzania 210 wanaoishi nchini humo ambao kati yao 171 ni wanafunzi na wengine ni maofisa wa ubalozi na raia wengine.

“Tunampongeza na kumshukuru Balozi wetu nchini Sudan, Silima Kombo Haji kwa kuendelea kufuatilia hali za Watanzania lakini Serikali inawahakikishia kuwa inachukua hatua stahiki za kuwarejesha ikibidi,” amesema.

Kwa mujibu wa Waziri, kusitishwa kwa mapigano hayo kwa muda wa saa 24 kuanzia jana saa kumi jioni, ni kutoa fursa kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu lakini akasema upo uwezekano wa kusitisha na mapigano na kuruhusu mazungumzo ya njia kwa amani.