Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Sangoma’ jela miaka 50 kwa kubaka, kumpa ujauzito mteja

Watu saba wafikishwa kortini wakidaiwa kujipatia Sh 428milioni mali ya Tanesco

Muktasari:

Mganga wa kienyeji, mkazi wa kijiji cha Nyaruyoba wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, Ibrahim Bukuru (41) amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kumpa mimba mteja wake aliyekwenda kupata matibabu.

Kibondo. Mganga wa kienyeji, mkazi wa kijiji cha Nyaruyoba wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, Ibrahim Bukuru (41) amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kumpa mimba mteja wake aliyekwenda kupata matibabu.

 Hukumu hiyyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Salah Mchalo wa Mahakama ya Wilaya ya Kibondo baada ya kuridhsihwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mchalo alisema mshtakiwa atatumia kifungo cha miaka 30 kwa kosa la ubakaji na miaka 20 kwa kosa la kumpa mimba mteja huyo ambaye ni wanafunzi.

Alisema ametoa hukumu hiyo baada ya ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo akiwemo daktari aliyefanya vipimo na kwamba hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo

Awali, mwendesha mashtaka wa polisi, Mwakanyamale Charles alidai tarehe tofauti za Agosti, 2021 katika kijiji cha Nyaruyoba mshtakiwa alimbaka mteja wake huyo mwenye umri wa miaka 18, aliyekuwa mwanafunzi katika Shule ya Selondari Lusumo mkoani Kagera. Alidai alimdanganya kuwa kufanya naye mapenzi ni sehemu ya tiba, ili kuondokana na changamoto aliyonayo.

Mwanafunzi hiyo alikuwa akiishi wilayani Ngara Mkoa wa Kagera na alisafiri hadi Kigoma kwa ajili ya matibabu ya kienyeji kutokana na magonjwa mbalimbali yaliyokuwa yakimsumbua ikiwemo mapepo.

Katika shtala la pili, mshtakiwa alidaiwa kumpa ujauzito mwanafunzi huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, hali iliyosababisha taharuki kwa wazazi na kufanya mwanafunzi huyo ashindwe kuendelea na masomo na kutimiza ndoto zake kwa ujumla.