Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu hukumu ya Mdude kusogezwa

Sababu hukumu ya Mdude kusogezwa

Muktasari:

  • Mbowe, wafuasi Chadema walifurika mahakamani kusikiliza hukumu hiyo bila mafanikio.

Mbeya. Shauku ya umati wa wafuasi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe kusikiliza hukumu ya kada wa chama hicho, Mdude Nyangali (32) jana ilizima ghafla baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kuahirisha kuisoma.

 Hukumu hiyo ya kesi ya kupatikana na gramu 23.4 za dawa za kulevya aina ya heroin imeahirishwa na Hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo, Zawadi Laizer ambaye aliahirisha “kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wake”.

Hakimu Laizer alipanga tarehe nyingine ya hukumu hiyo kuwa ni Juni 28 mwaka huu.

“Naomba kesi ya hukumu hii itasomwa tarehe tajwa kwani nimefanya jitihada za kutosha za kuhakikisha hukumu hii ingesomwa leo imeshindikana,” alisema bila kufafanua.


Ilivyokuwa

Mapema, kabla hakimu hajaingia kortini, viongozi wa Chadema waliokuwa ndani ya ukumbi wa mahakama waliongoza sala ya kumuombea Mdude ili Mungu amfanyie wepesi aachiwe huru.

Muda mfupi baada ya maombi kuisha Mdude akiwa na mtuhumiwa mwingine wakiwa wamefungwa pingu kitendo, ambacho kilimfanya mama yake mzazi kumkumbatia akiangua kilio.

Mdude alimtaka mama yake asilie akisema, “Mama mimi nitatoka, usilie mama yangu na wapiganaji wenzangu tuko pamoja, nitatoka tu.”

Kisha aliwageukiwa wafuasi wa Chadema, “ndugu zangu mbona mmepoa sana, kuna nini hapa, mimi nitashinda na nitatoka tu, msihofu kabisa,” alisema huku akiongozwa na askari polisi kwenda sehemu walipokaa Mbowe na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

Baada ya kuketi, Mdude alisalimiana na mama yake, kisha viongozi hao wawili.

Kauli ya Mbowe

Baada ya hukumu kuahirishwa, Mbowe aliwataka wafuasi wa chama hicho wawe na subira hadi tarehe iliyopangwa na makahama kutoa hukumu. “Ninaomba wanachama muwe watulivu kwani kwa imani haki itatendeka, naomba Juni 28 mjitokeze kwa wingi kama mlivyokuja

Awali, ilidaiwa kuwa Mei 11 mwaka jana Mdude Nyagali alipatikana na makosa mawili likiwepo la uhujumu uchumi na kupatikana na dawa ya kulevya aina ya heroin.