Barack, Michelle Obama wajibu mapigo madai ya kupeana talaka

Muktasari:
- Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama tangu Desemba mwaka jana hajaonekana hadharani akiwa ameambatana na mkewe Michelle Obama, jambo ambalo limeibua hisia na uvumi kuwa huenda wawili hao wapo kwenye mchakato wa kupeana talaka.
Wakati kukiwa na wingu la madai kwamba, Rais mstaafu wa Marekani, Barack na Michelle Obama wako kwenye mchakato wa kupeana talaka, wawili hao wameibuka na kuonyesha mapenzi yao hadharani.
Wawili hao wameonekena wakifurahia pamoja katika moja ya migahawa wanayoipenda ya Kiitaliano jijini Washington DC, Marekani.
Barack na Michelle walionekana wakitabasamu, huku wakipita kwenye mgahawa maarufu wa Osteria Mozza uliopo Georgetown mwishoni mwa wiki na kuwasalimia wateja, jambo ambalo limetajwa kuzima uvumi kuwa ndoa yao imekumbwa na dhoruba.

Tukio hilo linajiri wakati ambapo wanandoa hao wamelazimika kukanusha uvumi na tetesi kuwa wako mbioni kuachana.
Barack alionekana akitabasamu huku akiwasalimia wateja waliokuwa wakiwatazama kwa mshangao, huku Michelle akiwa mbele yake, akitembea kichwa akiwa ameinama, huku uso wake ukiwa na tabasamu.
Wateja wengine waliokuwa kwenye mgahawa huo walishangilia pindi walipowasili eneo hilo.
Obama aliwahi kuonekana akila chakula kwenye mgahawa huo maarufu jijini Washington siku moja kabla ya kuapishwa Rais Donald Trump. Michelle hakuambatana naye siku hiyo, wala hakuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Trump.

Michelle alionekana akiwa amependeza kwa suti ya rangi ya kijivu na suruali ya jeans, huku Barack akiwa amevalia fulana nyeusi na koti la rangi inayolingana.
Kabla ya kutoka pamoja safari hii, mara ya mwisho Barack kuonekana hadharani na Michelle ilikuwa Desemba, takriban miezi mitano iliyopita.

Hata hivyo, uamuzi wa Michelle kutohudhuria mazishi ya Rais wa zamani Jimmy Carter wala sherehe ya kuapishwa Rais Trump, vyote vilivyofanyika Januari, kukazua minong'ono kuhusu hali ya uhusiano wao wa kifamilia.
Hivi karibuni, Barack alikiri kwamba amekuwa akijitahidi kupunguza pengo kwa kufanya mambo ya kufurahisha pamoja naye