Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Samia apeleka neema Kizimkazi

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kufungua chumba cha Kompyuta na ukumbi wa mtihani wa Skuli ya Sekondari ya Muyuni B kwenye hafla fupi iliyofanyika Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar. Picha na Ikulu

Dar es Salaam. Neema yatawala Kizimkazi, hivi ndivyo inavyoweza kuelezwa kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani Makunduchi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la siku ya Kizimkazi eneo alilozaliwa kiongozi huyu wa Serikali ya awamu ya sita.

Maadhimisho ya Siku ya Kizimkazi kwa mwaka huu yalizinduliwa rasmi Agosti 26 na shughuli mbalimbali zimeendelea kufanyika kuelekea kilele chake kitakachofanyika Agosti 31.

Katika siku ya leo Agosti 29, Rais Samia amefanya ziara katika eneo hilo ambalo lipo ndani ya Wilaya ya Makunduchi, Mkoa wa Kusini, na kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo ya afya, elimu na biashara kwa ajili ya wakazi wa wilaya hiyo.

Miongoni mwa miradi iliyowekewa jiwe la msingi ni soko la samaki ambalo linajengwa kwa ufadhili wa benki ya CRDB, ujenzi wa shule ya watoto ya Tasani inayojengwa na benki ya NMB ambayo hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha Sh600 milioni.

Rais Samia pia amezindua ukumbi wa mitihani katika shule ya Sekondari Muyuni B, uliojengwa kwa ufadhili wa benki ya Azania, madarasa sita katika Shule ya Msingi Muyuni B, pamoja na kituo cha huduma za mama na mtoto kilichounganishwa na huduma ya M-MAMA inayotolewa na kampuni ya Vodacom.

Katika kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wilayani humo, Rais Samia amekabidhi magari mawili kwa ajili ya vituo vya polisi vya Makunduchi na Kizimkazi, ili viweze kutoa huduma kwa haraka pale inapohitajila.

“Tumejenga vituo vya polisi lakini tunaona kuna uhaba wa vitendea kazi, kwa hiyo nimemua kuunga mkono kwa kuleta magari. Maana kuna wakati matukio yanatokea au simu zinapigwa vituoni majibu ni kwamba hakuna usafiri, sasa hakutakuwa na maana ya kuwa na vituo kama hakuna usafiri, magari haya ni mapya ni matumaini yangu yatatunzwa,” amesema Rais Samia.