Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

 Mshua ashauri kinyesi cha wafungwa kitumike kutengeneza nishati ya kupikia magerezani

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Asha Abdallah Juma. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

  • Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Sh390.1 bilioni zimepokewa hadi Aprili, 2024 kwa ajili ya kujenga mfumo wa gesi vunde (biogesi) katika Magereza ya Kimbiji, Wazo Hill na Ngara.

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Asha Abdallah Juma ‘Mshua’ ameishauri Serikali itumie kinyesi cha wafungwa kama nishati ya kupikia kwenye magereza nchini ili kupunguza gharama za manunuzi ya gesi.

Ushauri huo ameutoa bunge leo Mei 15, 2024 wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka wa fedha 2024/25. Wizara imeliomba Bunge liidhinishe Sh1.7 trilioni.


Sehemu ya mtambo wa gesi ya kupikia unaotumia na kinyesi cha wanyama


“Nimeona hapa kumependekezwa kiasi kikubwa cha pesa kama Sh990 milioni kwa ajili ya kuandaa mitandao ya biogesi kwa kushirikiana na Taifa Gas na REA (Wakala wa Nishati Vijijini)”

“Lakini, napendekeza kwamba iweze kutumika biogesi ya kutumia vinyesi vya watu na vya wanyama.  Kwa kuwa magereza mengi yana mifugo mingi.  Magereza ni hazina ya kuonyesha nishati endelevu ya gesi ya kinyesi cha wafungwa na cha ng’ombe,” amesema.

“Mfano wa matumizi haya upo Rwanda. Kwa kutumia nishati hii itapunguza gharama za kuingia mikataba, pia itasaidia kuhifadhi mazingira kwenye magereza,” amesema.

Awali, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amelieleza Bunge kuwa katika kuondokana na matumizi ya kuni kwa kupikia chakula cha wafungwa na mahabusu magerezani, Jeshi la Magereza linatekeleza mkakati wa nishati safi.

Masauni amesema Sh390.1 bilioni zimepokewa hadi Aprili, 2024 kwa ajili ya kujenga mfumo wa gesi vunde (biogesi) katika Magereza ya Kimbiji na Wazo Hill mkoani Dar es Salaam, na Ngara (Kagera).

“Ununuzi wa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mifumo ya gesi vunde unaendelea na ujenzi wa mifumo hiyo umepangwa kukamilika Julai, 2024,” amesema.

Amesema Jeshi la Magereza limeandaa programu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo itatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu (2023/24 – 2025/26).

“Programu hii itagharimu Sh35.446 bilioni na itatekelezwa kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Utekelezaji utafanyika katika vituo 211 vya Jeshi la Magereza vinavyohusisha magereza 129, kambi za magereza 47, vyuo vinne na ofisi za magereza 31,” amesema.


Mfano wa Rwanda

Nchini Rwanda robo tatu ya nishati ya kupikia kwenye magareza inatokana na kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Naibu Kamishna Jenerali, Mary Gahonzire aliyenukuliwa na vyombo vya habari vya kimataifa, kutumia kinyesi cha binadamu imewasaidia kuokoa fedha nyingi.

Alisema kwa mwaka 2010 waliokoa Faranga za Rwanda milioni 800, mwaka 2011 waliokoa zaidi ya Faranga bilioni moja ambazo kwa ujumla ni zaidi ya Dola za Marekani 1.5 milioni (zaidi ya Sh3.8 bilioni).

Gahonzire alisema walikuwa na mpango wa kupanua huduma iweze kutumika kuwasha taa na matumizi mengine, badala ya nishati ya kupikia pekee.


Uzalishaji, matumizi mengineyo

Kwa wastani, mtu mzima hutoa kilo 91 za kinyesi na lita 730 za mkojo kwa mwaka. Taka za binadamu (kinyesi na mkojo) hazikutupwa huko Roma ya kale.

Majitaka hayo ambayo hayajatibiwa tangu miaka ya nyuma, yalitumika kama mbolea kwenye bustani. Wakati huohuo, mkojo ulitumiwa katika utengenezaji wa nguo.

Nyakati hizo pia kuna watu walikuwa wakizoa taka usiku na kuziuza kwa wakulima wa eneo hilo. Mkojo ulikusanywa na kutumika kulainisha ngozi.