Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Mikataba ya BIT haina tija katika Taifa’

Muktasari:

  • Serikali imeshauriwa kuwa makini na mikataba ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT), kutokana na madhara yake kiuchumi.

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikiwa imeshaingia katika mikataba 19 ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT), Mkurugenzi Muunganiko wa Mtandao wa asasi za kiraia na vyama vya wafanyakazi (TATIC), Olivier Costa ameonya kuwa mikataba aina hiyo haina tija kwa Taifa.

Akizungumza katika mjadala wa Twitter space ulioendeshwa na Mwananchi leo Agosti 02,2023 ukibebwa na mada ‘Je kuna tija yoyote kwa Tanzania kuendelea na mikataba ya uwekezaji wa nchi na nchi (BIT)?, Costa mikataba ya aina hiyo ina vitu vingi vinavyohitaji umakini ili kunufaika.

“Mikataba ya BIT ina vipengele vingi vinavyotufanya kama nchi tusiendelee ikiwemo hata kushindwa kufanya mabadiliko ya sheria.

“Hazina tija kwetu, kesi ni nyingi ambazo zinagharimu fedha nyingi, ambazo zingetumika kwenye maendeleo,” amesema.

Katika maelezo yake, Costa ametoa mfano wa wa kesi zote ambazo Tanzania imeshatikiwa fedha nyingi zilizotumika zilipaswa kuelekezwa kusaidia kwenye maendeleo.

“Kuna nchi ambazo zimeanza kutoka kwenye hii mikataba, kama ambavyo ilifanyika kwa mkataba wetu dhidi ya Uholanzi, hili linaweza kufanyika kwa BIT nyingine,” ameshauri.

Naye Mshauri wa Biashara za Kimataifa na Uwekezaji, Jackson Roselian amesema uwepo wa mikataba ya aina hiyo, hakuangaliwi wawekezaji.

“Kikubwa wanachoangalia ni tija atakayopata kutokana na uwekezaji na hali ya usalama. Hakuna ushahidi wa kutosha kwamba mikataba ya BIT inavutia wawekezaji,” amebainisha.