Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katibu Mkuu UVCCM amewataka vijana kuilinda amani ya nchi

Katibu Mkuu UVCCM amewataka vijana kuilinda amani ya nchi

Muktasari:

  • Kihongosi amesema amani ikipotea watakaoumia katika kuitafuta ni vijana wenyewe hivyo asiwepo wa kufanya mzaha katika kuilinda

Dodoma. Vijana wa Tanzania wamekumbushwa jukumu la kulinda amani kwamba liko mikononi mwao hivyo hawatakiwi kumwachia mtu mwingine kwa kuwa amani ikitoweka watabeba mzigo kuitafuta.

Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Kenani Kihongosi wakati akizindua mazoezi ya jogging kwa vijana jijini Dodoma ambayo ameagiza yaende nchi nzima.


Kihongosi amesema vijana ndiyo jicho la nchi yoyote katika suala la ulinzi hivyo ikitokea amani inatoweka watakaokuwa wa kwanza kubebeshwa lawama hizo watakuwa ni wao.


Amewataka kuwa makini na kujibu mapigo kwenye mitandao hasa jumbe zinazolenga kuwachafua na kuwadhalilisha viongozi wa Serikali na Taifa kwa ujumla.


Hata hivyo amesema wakati wanajibu mambo hayo ni vema wakawa na staha ili wasiwe chanzo cha kuivuruga amani ambayo ikipotea namna ya kuipata inakuwa ni ngumu zaidi.


Kihongosi huyo ameagiza viongozi wa UVCCM mikoani kuanzisha mpango wa mazoezi ili kuwakusanya vijana pamoja katika kujiimarisha na kuijenga miili yao iweze kukabiliana na suala zima la magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa corona.


Kingine amezungumzia chanjo ya corona akiwataka Watanzania kupuuza kauli za baadhi ya watu kuwa haifai kwa matumizi ya ambapo amesema ni bora akili ya kuambiwa mtu akachanganya na yake kwa kuwa wengi wanaosema kuhusu chajo hiyo ni kwa sababu hayajawafika.