Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Jitokezeni kuchangia damu kuokoa maisha’

Kiongozi wa ukusanyaji damu salama, Rose Bulemo akimtoa damu Abdul Nasir jijini Dar es Salaam. picha na Pamela Chilongola

Muktasari:

  • Katika kampeni ya kuelekea miaka 20 ya uchangiaji wa damu nchini, Mpango wa Taifa wa Damu Salama unatarajia kukusanya chupa lita 1,120 za damu

Dar es Salaam. Mpango wa Taifa wa Damu Salama unatarajia kukusanya chupa za damu lita 1,120 katika maadhimisho ya kuelekea siku ya uchangiaji damu.

 Mpango huo umewaomba watu wenye makundi O, A na B Negative wajitokeze kuchangia damu, kwa kuwa makundi hayo hupatikana kwa nadra, ili wenye huitaji huo waweze kusaidiwa.

Akizungumza leo Jumanne  Juni 11, 2024, Ofisa Uhamasishaji Damu Salama Kanda ya Mashariki, Evelyn Dielly amewaomba Watanzania wajitokeze kuchangia damu kwa hiari kwa kuwa wagonjwa wenye uhitaji wa damu ni wengi.

"Leo tunajumuika na Benki ya Equity katika kampeni ya kuelekea miaka 20 ya uchangiaji wa damu, hivyo tunawahusisha wadau wote wajitokeze kwa kuwa kiwanda cha kuzalisha damu ni sisi wenyewe itawasaidia wagonjwa wakiwamo na wajamzito waliopata ajali," amesema Dielly.

Amesema kati ya watu 100 wanaojitokeza kuchangia damu, ni watano tu ndio huwa na makundi ya O, A na B Negative.

Meneja Mwandamizi wa Rasilimaliwatu wa Benki ya Equity, Fatma Msofe amesema benki hiyo imeamua kusaidia Serikali katika uchangiaji wa damu salama.

"Kama tunavyojua damu huwezi ukazalisha kiwandani, hivyo tunawaomba watu wajitokeze katika maadhimisho ya kuelekea siku ya uchangiaji damu ili tuweze kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji," amesema Msofe.

Abdul Nasri aliyejitokeza kuchangia damu, amesema amehamasiaka kuchangia kwa sababu mahitaji ya damu ni makubwa kwa wajawazito na watu waliopata ajali.