Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Walichokubaliana ANC na DA

Muktasari:

  • Chama cha ANC kimeingia mkataba na DA kuunda Serikali ya Afrika Kusini, ambapo Ramaphosa ataendelea kuwa rais katika muungano huo.

Johannesburg. Chama cha African National Congress (ANC) kimeingia mkataba na Democratic Alliance (DA) kuunda Serikali ya Afrika Kusini, wakikubaliana vipaumbele tisa kikiwamo cha ukuaji wa uchumi.

Mengine ni upatikanaji wa ajira, kuboresha upatikanaji na ubora wa huduma za msingi, kukabiliana na gharama kubwa za maisha na kutoa huduma bora za afya zinazopatikana.

Mengine ni kuunda huduma za umma zisizo na rushwa, kuimarisha utekelezaji wa sheria kukabiliana na masuala kama uhalifu na ukatili wa kijinsia na kutoa usalama wa kijamii.

Katika makubaliano hayo, Ramaphosa ataendelea kuwa Rais katika muungano huo, huku nafasi nyingine zikiendelea kujadiliwa.

Mbali na DA, ANC imekiingiza pia Chama cha Wazalendo wa Kizulu, Inkatha Freedom Party katika umoja huo, huku vyama uMkhonto weSizwe (MK) cha Rais wa zamani, Jacob Zuma na Economic Freedom Fighters (EFF), vilivyokuwa katika nafasi ya tatu na ya nne vikibaki nje ya muungano.

Mapatano hayo yamekuja zikiwa zimepita mbili tangu uchaguzi kufanyika Mei 29, 2024 ukishindwa kutoa mshindi atakayeunda Serikali.

Kwa mara ya kwanza tangu Serikali ya Wazungu wachache kusitishwa mwaka 1994, Chama cha ANC kilishindwa kufikisha asilimia 50 ya kura na kupata asilimia 40.2, kikifuatiwa na DA (asilimia 22), MK (asilimia 15) na EFF (asilimia 9.5).

Akizungumza na Shirika la Habari la Reuters leo Juni 14, 2024, mpatanishi wa DA, Helen Zille amesema mkataba umesainiwa kuunda serikali ya mseto.


Kiongozi wa DA

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Viwanja vya Bunge la Afrika Kusini, Kiongozi wa DA, John  Steenhuisen amesema mpaka sasa hakujawa na makubaliano kuhusu nafasi za baraza la mawaziri yaliyofikiwa na mazungumzo hayo yataanza hivi karibuni.

"Tunatambua kuna haja ya kujumuisha demokrasia na Rais atazingatia hili wakati anateua baraza lake la mawaziri.

"Leo tutamuunga mkono Rais Ramaphosa, nayo ANC itamuunga mkono mgombea wetu kwa naibu spika," amesema Steenhuisen akikaririwa na BBC.

Ingawa Steenhuisen amebainisha umuhimu wa makubaliano hayo, pia amesema matatizo ya Afrika Kusini, kama uhalifu na masuala ya uchumi, hayatatatuliwa mara moja na kwamba na kwamba njia itakuwa ngumu.

"Watu wametuambia kuwa wakati wa siasa mpya za ushirikiano na utatuzi wa matatizo umefika," Steenhuisen amesema.

"Kuanzia leo DA itatawala Jamhuri ya Afrika Kusini kwa roho ya umoja na ushirikiano. Tunafanya hivyo kwa ajili ya mamilioni waliotupigia kura na Waafrika Kusini wote wanaotamani serikali bora," ameongeza.


Imeandikwa kwa ushririkiano na Mashirika ya Habari