Ufaransa yapiga marufuku kuvaa abaya shuleni

Ufaransa. Serikali nchini Ufaransa imetangaza marufuku kwa wanafunzi wa kike wa shule za umma kuvaa vazi aina ya abaya ambalo huvaliwa mara nyingi na wafuasi wa dini ya Kiislamu nchini humo.
Marufuku hiyo itaanza Septemba 4, 2023 baada ya muhula mpya wa masomo wan chi hiyo kuanza rasmi.
Hatua hiyo inakuja baada ya Ufaransa kupiga marufuku alama za kidini katika shule za serikali na majengo ya serikali, ikisema kwamba zinakiuka sheria za kilimwengu.
Hata hivyo, nchini humo kuvaa hijab kwa msichana katika shule za Serikali kumepigwa marufuku tangu 2004 katika shule zinazomilikiwa na serikali.
"Unapoingia darasani, hupaswi kuwa na uwezo wa kutambua dini ya wanafunzi kwa kuwatazama tu," Waziri wa Elimu Gabriel Attal aliiambia TF1 TV ya Ufaransa, na kuongeza: "Tumeamua kwamba abaya haiwezi kuvaliwa tena. shuleni."
Hatua hiyo inajiri baada ya miezi kadhaa ya mjadala kuhusu uvaaji wa abaya katika shule za Ufaransa.
Ukiachilia mbali tu katazo hilo kuwahusu wanafunzi wa shule za umma lakini mwaka 2010 nchi hiyo ilipiga marufuku uvaaji wa vazi la kiislamu linalofunika uso wa mwanamke maaruf kama ‘nikab’ hadharani jambo ambalo liliibua hasira kwa watu wa Imani hiyo.