Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump awatangazia kiama watakaosababisha vurugu magari ya Tesla

Muktasari:

  • Mbali ya kununua Rais Trump ametoa onyo kali kwa wote watakaothubutu kushambulia au kuleta vurugu kwenye magari hayo pamoja na maduka yake, akisema itahesabika kama ugaidi hivyo wahusika watakiona cha mtemakuni.

Marekani. Wakati Hisa za magari ya Tesla zikianza kuongezeka kwa karibu asilimia nne baada ya anguko, Rais wa Marekani, Donald Trump amezipigia chapuo gari hizo za umeme akinunua kwa ajili ya wafanyakazi wake.

Mbali ya kununua, Rais Trump ametoa onyo kali kwa wote watakaothubutu kushambulia au kuleta vurugu kwenye magari hayo pamoja na maduka yake, akisema itahesabika kama ugaidi hivyo wahusika watakiona cha mtemakuni.

Hatua hiyo inatajwa sehemu ya kumuunga mkono tajiri Elon Musk ambaye ni mshirika wake wa karibu zaidi. Musk kwa sasa anaongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali ya Trump, inayojulikana kama Doge.

"Ukifanya hivyo kwa Tesla, au kwa kampuni yoyote, tutakukamata, na utapitia mateso makali," Trump ameongeza kwa mujibu wa India Today.

Msemaji wa Ikulu, Harrison Fields amesema mashambulizi yanayoendelea dhidi ya Tesla yanayofanywa na wanaharakati wa mrengo wa kushoto wenye msimamo mkali ni ugaidi wa ndani.

Katika maandamano ya hivi karibuni watu 350 walikusanyika nje ya duka la Tesla huko Portland, Oregon, huku wengine tisa wakikamatwa katika maandamano ya New York mapema Machi.

Pia, kumekuwa na ripoti za vyombo vya habari kuhusu uharibifu wa magari na maduka ya Tesla, ambao kwa sasa uchunguzi unaendelea.

Kikundi kinachosema kinaandaa maandamano ya ‘Tesla Takedown’ kilijibu kupitia mtandao wa kijamii wa Bluesky, kikisema kuwa maandamano yao ni ya amani na yanapinga vurugu.

Rais Trump alitangaza ununuzi wa Tesla Model S, ambayo huanza kuuzwa kwa karibu dola 80,000, kama ishara ya kumuunga mkono Musk.

Aidha, kwa mujibu wa Reuters Trump amesema vurugu dhidi ya maduka ya Tesla zitaorodheshwa kama ugaidi wa ndani, na wahusika watapitia mateso makali.

"Wanaharibu kampuni kubwa ya Marekani," Trump amesema akiwa Ikulu huku karibu yake kukiwa na magari kadhaa ya Tesla yalikuwa yamepangwa kwenye barabara kati ya jumba la Ikulu na Lawn ya Kusini.