Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi watumia risasi za mpira, Ruto ataka mazungumzo

Rais wa Kenya, William Ruto wakati akihutubia Taifa mubashara kuhusu maandamano nchini humo Juni 25, 2024.

Muktasari:

  • Asasi ya kiraia ya haki za binadamu inayotambuliwa na Serikali ya Kenya imebainisha idadi ya vifo vya watu 22 kote nchini, 19 jijini Nairobi pekee, baada ya maandamano ya Jumanne na kuapa kufanya uchunguzi.

Nairobi. Licha ya Rais William Ruto kufutilia mbali muswada wa Sheria ya Fedha uliopendekeza Ongezeko la Kodi, vijana nchini Kenya leo Alhamisi Juni 27, 2024 wameendelea kuandamana huku polisi wakiwafyatulia risasi za mpira na mabomu ya machozi.

Maandamano hayo yakiongozwa na vijana maarufu Gen Z, yamezipuuza mamlaka na Serikali ya Ruto ikabaki njiapanda, kati ya kuchukua msimamo mkali kudhibiti machafuko au kutaka mazungumzo.

Makumi ya waandamanaji walikusanyika katikati mwa jiji la Nairobi huku wanajeshi na polisi waliovalia zana za kuzuia ghasia wakizuia njia zote za kuelekea Ikulu na bungeni, kwa mujibu wa AFP.

Maofisa wa polisi waliwafyatulia risasi za mpira na mabomu ya machozi makundi madogo ya waandamanaji na kuwakamata takriban watu saba huku vurugu zikizuka na baadhi ya waandamanaji wakiwarushia askari hao mawe.

"Vijana hawatapumzika,” Lucky, mhitimu wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 27, ameiambia AFP.

“Tunapigania mustakabali wetu,” amesema, akiongeza kuwa hana imani na Ruto ambaye awali aliwafananisha waandamanaji na “wahalifu” kabla ya kuwaunga mkono.

Maduka mengi yamefungwa kwa sababu ya wafanyabiashara kuhofia machafuko.

Vijana hao pia waliandamana katika mji wa Mombasa na ngome ya upinzani ya Kisumu, ambako wengine wamefunga barabara na kuwasha moto katika mji huo ulio mwambao mwa Ziwa Victoria.

Baada ya majengo ya Bunge kuvamiwa Jumanne iliyopita na polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji, Ruto alibadilisha msimamo kuhusu ongezeko la kodi lililochochea maandamano hayo na kukataa saini sheria ya ongezeko hilo.

Hata hivyo, waandamanaji wameshikilia msimamo wao wa kuandamana leo Alhamisi kuwakumbuka waliouawa katika maandamano hayo, wakisema uamuzi wa Ruto kubadilisha msimamo ni jambo dogo na amechelewa.

Asasi ya kiraia ya haki za binadamu inayotambuliwa na Serikali ya Kenya imesemaa idadi ya vilivyotokana na maandamano hayo kote nchini ni 22, kati ya hivyo 19 vikitokea Nairobi pekee.

“Hii ndiyo idadi kubwa zaidi ya vifo katika maandamano ya siku moja,” amesema Roseline Odede, mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya inayomilikiwa na  Serikali, akiongeza kuwa watu 300 walijeruhiwa kote nchini humo.

Maduka yamefungwa kwa sehemu kikubwa katikati ya jiji la Nairobi leo Alhamisi Juni 27, 2024.

“Hatuwezi kujihatarisha. Hatujui nini kitafuata,” amesema Joe, mfanyakazi katika duka la manukato, alipokuwa akijiandaa kuelekea nyumbani.

“Kwa nini walilazimika kuwaua vijana hawa? Muswada huu haufai hadi kwa watu kufa,” kijana huyo wa miaka 30 amesema.