Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Netanyahu: Vita inatugharimu sana lakini hatuna budi kuendelea kupambana

Muktasari:

  •  Waziri Mkuu wa Israel amesema vita kati kati ya nchi hiyo na Hamas vinaleta madhara kwa wanajeshi wake lakni ameahidi kusonga mbele zaidi.

Gaza. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema vita vinayoendelea Gaza kati yao na Hamas vinawagharimu na idadi ya wanajeshi wanaouawa kwenye mapigano hayo inazidi kuongezeka.

Shirika la Habari la AFP limemnukuu Netanyahu wakati akizungumza leo Jumapili Desemba 24 baada ya jeshi la nchi yake kutangaza kuuawa kwa wanajeshi 14 wa nchi hiyo ndani ya siku mbili Desemba 22 na 23.

“Hii ni asubuhi ngumu, baada ya siku ngumu sana ya mapigano huko Gaza. Vita vinaleta gharama kubwa sana... lakini hatuna budi kuendelea kupigana," ameongeza katika taarifa yake.

Waziri Mkuu huyo amesema "vita vinatuletea madhara makubwa sana lakini hatuna chaguo, ila kuendelea kupigana."

Wakati huohuo, tovuti ya Times ya Isarel imeripoti kuwa wanajeshi hao wa IDF wamekufa katika mapigano makali kusini na katikati mwa Gaza.

Taarifa zaidi zinasema wanajeshi 153 wameshauawa tangu Israel ilipoanza operesheni ya mapigano ya ardhini Oktoba 27.

Netanyahu amesisisitiza kuwa wanaendelea kwa nguvu hadi watakapofikia malengo yao yote ya kuiharibu Hamas, kuwarejesha mateka na kuhakikisha Gaza haitakuwa tena tishio kwa Israeli.

Aidha amesisitiza kuwa vita hivyo vitakuwa vya muda mrefu hadi pale Hamas itakapoondolewa.

Vifo Gaza vyapaa

Wizara ya Afya ya Gaza imesema kwamba takriban watu 20,424 wameuawa katika eneo la Palestina tangu kuanza kwa vita na Israeli. Idadi hiyo ilijumuisha vifo 166 vilivyotokea katika muda wa saa 24 zilizopita.

Oktoba 7, 2023 Hamas ilivamia Israel na kuua takriban watu 1,140 kuteka wengine zaidi ya 250, ambapo kati yao 105 wameachiliwa na wengine wameuawa wakiwemo Watanzania wawili.  Hadi leo ni siku ya 79 tangu vita hivyo vianze.