Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neno ‘umwagaji damu’ linavyomtesa Trump, Biden ahamaki kura za maoni

Muktasari:

  • Kauli ya Donald Trump kwamba asiposhinda uchaguzi wa Novemba kutatokea umwagaji damu,  imemtesa kiasi cha wafuasi wake kutoa tafsiri nyingine kwamba alikuwa na maana ya janga la kiuchumi, huku mpinzani wake Rais Joe Biden akiendelea naye kulizwa kwenye kura za maoni.

Washington. Wakati neno ‘bloodbath’ au ‘umwagaji damu’ lililotumiwa na Donald Trump likileta taharuki na kuibua  tafsiri mbili tofauti, mpinzani wake,  Rais Joe Biden naye amehamaki na kutoa kiapo alipoambiwa idadi ya kura zake za maoni,  imezidi kupungua kwa madai ya kushindwa kushughulikia mzozo wa Israeli na Hamas.

Trump akihutubia mkutano wa hadhara huko Dayton, Ohio Jumamosi ya Machi 16, 2024 pia amenukuliwa akiwaita wahamiaji ni ‘wanyama’, wahalifu na nyoka waliovamia Marekani.

Kauli ya Trump ya kubashiri machafuko ya umwagaji damu iwapo atashindwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Marekani utakaofanyika  Novemba 5, 2024,  imeleta mjadala ambapo wafuasi wake wamevilaumu vyombo vya habari kwa kupotosha huku wengine wakiamini amemaanisha umwagaji damu.

“Kama sitachaguliwa, itakuwa ni umwagaji damu kwa watu wote. Itakuwa ni umwagaji damu kwa nchi,” amenukuliwa Trump (77) akionya kwenye mkutano huo wa hadhara.

Neno umwagaji damu limechukuliwa na vyombo vya habari kwamba kiongozi huyo pengine anaamanisha akishindwa uchaguzi, kutatokea vurugu za kisiasa zitakazosababisha umwagaji damu.

Hata hivyo, msemaji wa timu ya kampeni ya Trump, Steven Cheung amesema Trump kwenye hotuba yake ametumia neno ‘umwagaji damu’ akiwa na maana kutakuwa na janga la kiuchumi,  iwapo Biden ataendelea kuwa madarakani kutokana na ongezeko la viwanda vya magari kutoka China.

Pia, baadhi ya wafuasi wake wamelalamikia vyombo vya habari kwa kuchukua neno la ‘umwagaji damu’ pekee badala ya kuangalia muktadha mzima wa aliyoyasema.

Msemaji wa timu ya kampeni ya Biden, James Singer yeye amemshutumu Trump kwamba amekuwa mtu wa vitisho vya vurugu vya kisiasa kwa mara nyingine.

“Anataka Januari 6 nyingine, lakini watu wa Marekani wanaenda kumbwaga tena kwenye uchaguzi wa Novemba kwa kuwa wanaendelea kuwakataa wanaharakati wenye msimamo mkali, anapenda vurugu, ana kiu ya kulipa kisasi,” amesema Singer.

Kauli ya umwagaji damu pia imemuibua mkurugenzi msaidia wa zamani wa Shirika la Kijajusi la Marekani (FBI), Frank Figliuzzi ambaye ameandika kwenye akaunti yake ya X zamani Twitter kwamba;

“Trump amesema kama hatachaguliwa kutakuwa na umwagaji damu kwenye nchi. Kama atachaguliwa, pia itakuwa ni umwagaji damu itategemea na dhamira. Uchaguzi ni wazi ni tishio.”

Pia, Spika wa zamani wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi naye kuhusiana na kauli ya Trump amekiambia kituo cha televisheni cha CNN kuwa:
“Ni lazima tushinde uchaguzi kwa sababu amebashiri umwagaji damu. Hii ina maana gani? Atakachofanya ni umwagaji damu? Kuna kitu kibaya hapa.”


Alichosema Trump

Akihutubia wafuasi wake huko Ohio, Trump amesema Mexico kwa zaidi ya miaka 30 wamekuwa wakifanya biashara ya magari Marekani.

“China sasa inajenga viwanda vingi vya kutengeneza magari Mexico, na wanafikiri watauza hayo magari Marekani bila kulipa ushuru mpakani. Ngoja niwaambie kitu kuhusu China. Ukimsikiliza Rais Xi (Jinping), na rafiki zake, lakini wanaelewa njia nitakazotumia.

“Hivyo viwanda vikubwa vya kutengeneza magari vinavyojengwa Mexico sasa, kama mnadhani mtayauza Marekani basi tutaweka asilimia 100 ya ushuru kwa kila gari litakalovuka mpaka,” alisema na kuongeza:

“Kama sitachaguliwa, itakuwa ni umwagaji damu kwa watu wote. Itakuwa ni umwagaji damu kwa nchi.’’
Mmoja wa viongozi wa chama cha Republican cha Trump, Mike Turner akihojiwa na televisheni ya ABC,  amesema kauli ya Trump imelenga kuwepo janga la kiuchumi na si umwagaji damu.


Kauli ya Trump kuhusu wahamiaji

Akizungumzia ongezeko la wahamiaji,  Trump amesema hao ni wahamiaji wahalifu wako kama nyoka.

“Sasa tuna aina mpya ya uhalifu. Ninauita uhamiaji wa uhalifu wa Biden, lakini ndefu mmno tuite tu uhalifu wa uhamiaji.

“Duniani kote sasa uhalifu haupo, unajua kwa nini? Kwa sababu wamewaleta kwetu wahalifu. Venezuela umeshuka hadi asilimia 66 kwa sababu wametuletea magenge ya wahalifu,” amesema.

Amesema wanaoumia na uvamizi wa wahamiaji ni Wamarekani wenye asili ya Afrika na Wamarekani wenye asili ya Hispania,  kwa sababu wahamiaji wanachukua kazi za Wamarekani.


Tahamaki ya  Biden

Wakati Trump akisema hayo,  Rais Joe Biden naye amekumbwa na hamaki na kutoa kiapo alipoambiwa idadi ya kura zake za maoni zimezidi kupungua,  kwa madai ya kushindwa kushughulikia mzozo wa Israeli na Hamas.

Kura za maoni za Biden zinaonyesha zimeshuka baada ya kutoa hotuba ya mwaka ya ‘State of the Union’  wiki iliyopita hadi kufikia asilimia 37.4. Kabla ya hotuba hiyo kwa maana mwishoni mwa Januari, Trump alikuwa na asilimia 45 na Biden asilimia 44.

Mwanzoni mwa Machi kuanzia tarehe 8-11 Trump ameongeza kura na kufikia 46 wakati Biden akiwa na asilimia 44. Kura za kumuidhinisha pia zilishuka kutoka asilimia 40 hadi asilimia 39.