Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump kizimbani leo, tuhuma kuingilia uchaguzi Georgia

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump

Muktasari:

  • Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na washtakiwa wenzake 18 akiwemo wakili wake Rudy Giuliani na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa nchi hiyo, Mark Meadows wanatarajiwa kusomewa mashtaka yao leo Jumatatu Agosti 28, 2023 kwa mara ya kwanza.

Georgia. Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na washtakiwa wenzake 18 akiwemo wakili wake Rudy Giuliani na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa nchi hiyo, Mark Meadows wanatarajiwa kusomewa mashtaka yao leo Jumatatu Agosti 28, 2023 kwa mara ya kwanza.

Trump anakabiliwa na mashtaka ya tuhuma za kuingilia uchaguzi wa Georgia kwa madai ya kutafuta kura 11,000 za kumzidi aliyekuwa mpinzani wake katika uhaguzi wa mwaka 2021, Joe Biden.

Miongoni mwa mashahidi wanaosubiriwa kutoa ushahidi siku ya leo ni pamoja na Katibu wa Jimbo la Georgia Brad Raffensperger, ambaye anadaiwa kupokea alipokea simu Januari 2021 kutoka kwa Trump kwa ajili ya kuombwa amtafutie kura ili ashinde katika uchaguzi huo.