Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya Trump yaangukia pabaya, alalamika kuhujumiwa

Georgia. Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump imepangwa kusikilizwa tena Machi 4, 2024 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi wa ndani ya chama chake cha Republican wa kumchagua mgombea Urais.

Trump na Mawakili wake wamedai kuhujumiwa na wapinzani wake wa kisiasa kwani tarehea ambayo kesi imepangwa kusikilizwa atakuwa katika mchuano mkali wa kisiasa akiwania kurudi tena Ikulu kwa mara ya pili.

Trump anatuhumiwa kumlaghai Ofisawa Uchaguzi katika Jimbo la Georgia ili aweze kumuongezea kura ili amshinde aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi wa mwaka 2020, Joe Biden wa chama cha Democratic.

Mawakili wa Trump tayari wamelalamika kuhusu mapendekezo ya ratiba ya kesi zinazokinzana na kampeni ya urais za mteja wao huku baadhi ya wafuasi wa Trump wakitaja kitendo hiko kuwa ni "kuingilia uchaguzi".

Hata hivyo, Trump amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo. Katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii, alikejeli maamuzi ya Hakimu huyo akiyataja ni ya kumkomoa na yamepangwa na Serikali iliyopo madarakani.

Awali timu ya wanasheria wa Trump ilikuwa imependekeza kesi hiyo isikilizwe tena Aprili 2026 hata hivyo hakimu alikataa