Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mmoja auawa, wengine wakamatwa kufuatia ghasia Kenya

Muktasari:

  • Maandamano yameendelea sehemu mbalimbali nchini Kenya huku kikiripotiwa kifo cha mtu mmoja kilichotokana na majeraha ya risasi kutokana na maandamano yanayoendelea nchini humo.

Kenya. Mtu mmoja amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi katika maandamano yanayoendelea nchini Kenya, kutokana na vurugu zilizozuka kati ya polisi na waandamanaji eneo la Emali, Kaunti ya Makueni.

 Kwa mujibu wa mtandao wa Nation, waandamanaji hao wamechoma gari la polisi na kurusha mawe kwenye majengo ya benki na kusababisha shughuli mbalimbali za kiuchumi kusimamia.

Jijini Nairobi, mamia ya vijana wameanza kukusanyika katika uwanja wa Kamkunji jijini Nairobi ambapo viongozi wa upinzani watafanya mkutano kabla ya kuanza maandamano mitaani.

Polisi jijini humo walijaribu kuwatawanya watu hao ili wasikusanyike katika viwanja hivyo kwa kutumia mabomu ya machozi, hata hivyo, walionekana baada ya watu hao kuwazidi nguvu polisi.

Katika harakati za makabiliano kati ya polisi na wafuasi hao wa upinzani, baadhi ya vijana waliwarushia mawe maafisa wa polisi ambapo maafisa hao waliondoka mara moja katika eneo hilo.

Wafuasi hao wanaodaiwa kumuunga mkono Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini humo, Raila Odinga wameapa kuendelea na mkutano wao huku wakiwaonya polisi kutowaingilia.

"Tunataka kuwa na maandamano ya amani lakini inaonekana polisi wanataka matatizo," alisema Peter Musau mmoja wa waandamanaji.

Kwa upande mwingine, waandamanaji hao wanaoipinga Serikali, wamedaiwa kujihusisha na uporaji. Pia wameonekana wakiharibu miundombinu pembeni mwa barabara eneo la Mlolongo.

Nakuru nako kumeripotiwa moshi mzito ukionekana huku ghasia za waandamanaji hao zikiendelea maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo, ambapo taarifa za kiusalama zimesema watu kadhaa wamekamatwa kutokana na ghasia hizo.