Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Israel, Palestina vifo vyakaribia 1,000

Muktasari:

  • Maofisa wa pande zote mbili zinazopigana wamesema kuwa idadi ya waliouawa imeongezeka hadi karibu 1,000 mpaka hivi sasa tangu kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas kuanzisha mashambulizi yake ya kushtukiza dhidi ya Israel hapo jana kwa mfululizo wa makombora ya angani na ardhini huku Israel ikijibu mapigo.

Israel. Maofisa wa pande zote mbili zinazopigana wamesema kuwa idadi ya waliouawa imeongezeka hadi karibu 1,000 mpaka hivi sasa tangu kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas kuanzisha mashambulizi yake ya kushtukiza dhidi ya Israel kwa mfululizo wa makombora ya aangani na ardhini.

Shirika la Habari la AFP limeandika taarifa kuwa kuna vifo vya zaidi ya watu 600 upande wa Israel, ofisi ya vyombo vya habari vya serikali imesema, huku maofisa wa Gaza wakiripoti vifo vya watu 370, na maelfu ya wengine kujeruhiwa kila upande.

Maelfu ya vikosi vya Israel vimetumwa kupambana na wanamgambo wa Hamas kusini mwa nchi hiyo na jeshi la anga limeshambulia ukanda wa Gaza huku Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akionya uwezekano wa vita kuwa na muda mrefu na ngumu.

"Tutawafikia kila mtu hadi tutakapomuua kila gaidi nchini Israel," ameapa msemaji wa kijeshi Daniel Hagari, siku moja baada ya mamia ya wapiganaji wa Hamas kuingia Israel kwa kutumia magari pamoja na boti.

Israel pia imeshambuliwa kutoka kaskazini wakati wanamgambo wa Hezbollah kutoka Lebanon waliporusha makombora na risasi leo Jumapili. Israel imeshajibu kwa mashambulio ya mizinga katika mpaka unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

"Tunapendekeza Hezbollah kutoingia katika hili, ikiwa watakuja, tuko tayari."


Sute Kamwelwe kwa msaada wa mtandao