Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hamas yatangaza kuwaua mateka wa Israel

Muktasari:

  • Kufuatia mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza hususani yale yaliyolenga raia, Kundi la Kipalestina la wanamgambo wa Hamas linaloendelea na mapigano dhidi ya Israel limetishia kuwaua mateka wa Israel walio chini yao.

Gaza. Kundi la Kipalestina la wanamgambo wa Hamas linaloendelea na mapigano dhidi ya Israel limetishia kuwaua mateka wa Israel walio chini yao.

 Hamas limesema kitendo cha Israel kuwalenga raia katika eneo la Gaza kinachochea hasira zaidi na kuonya kwamba kila wakati Israel inapopiga eneo hilo na Hamas wataua mateka mmoja.

Katika ujumbe wa sauti uliotolewa jana Jumatatu, Abu Obeida, msemaji wa Qassam, ameeleza mashambulizi makali yametokea katika maeneo ya kiraia huko Gaza, eneo la pwani lenye wakazi wengi ambalo limezingirwa katika miaka kadhaa tangu Hamas kuchukua mamlaka.

Muda mfupi baada ya kauli ya Obeida, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alionya kwamba picha za uharibifu na zilizosambaa kutoka ngome za wanamgambo wa Hamas  ni mwanzo wa kile wanachotegemea kukifanya.

"Tunatangaza kwamba kila shambulio linanalolenga watu wetu majumbani mwao, litafidiwa kwa kuuawa kwa mateka wa raia wa adui zetu," Obeida  alisema huku akisema mauaji hayo yatarushwa kwa sauti na video.

Wakati jumla ya vifo ikifita 1,500 kwa pande zote mbili, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa nchi yake iko kwenye vita ambavyo haikuvianzisha na kusisitiza kwamba kikundi cha wanamgambo cha Hamas kijiandae kulipa gharama ambayo haitasahaulika maishani mwao na kwa maadui wote wa Israel na ni lazima Israel itashinda vita hivyo na ikishinda basi dunia nzima itashinda.

Aidha Netanyahau ameongeza kwamba vita hivyo wamelazimishwa katika njia ya kikatili zaidi na itahakikisha inavimaliza na maadui zao wakae wakijua kwamba kwa kuivamia Israel wamefanya makosa makubwa kwani imepelekea vifo kwa raia wasiokuwa na hatia, kuua vijana waliokuwa kwenye tamasha, kuchinja familia za Waisraeli pamoja na kuteka raia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema anasikitishwa na amri ya Israel ya kuzingira Gaza na kukata umeme, chakula na mafuta katika eneo hilo lenye wakazi wengi.

Pia amelaani mashambulizi ya makombora ya hospitali na makazi katika Ukanda wa Gaza, akiomba Umoja wa Mataifa uruhusiwe kuingia kutoa misaada ya kibinadamu.

Guterres alizungumza na vyombo vya habari jana baada ya kukutana na viongozi wakuu, akilaani kitendo cha Hamas kuwateka mateka, raia na wanajeshi na pia alielezea wasiwasi wake juu ya ripoti za zaidi ya Wapalestina 500 waliouawa huko Gaza.

Aliionya Israel kwamba operesheni za kijeshi lazima zifanywe kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.