Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Black Dolphin: Gereza hatari duniani lililopo Russia

Muktasari:

  • Makosa wanayofungwa watu katika gereza hilo ni pamoja na ugaidi, wanaolawiti na kunyanyasa watoto wadogo.

Urusi. Kusini, Kaskazini mwa Russia, katika Jiji la Sol-Iletsk, karibu kabisa na mpaka wa Khazakhstan na Russia, ndipo linapopatikana gereza liitwalo Black Dolphin (Pomboo mweusi), ambalo linatajwa kuwa moja ya magereza hatari zaidi duniani.

 Kwa mujibu wa maofisa wanaotetea haki za binaadamu, Black Dophin lipo kwenye orodha ya tatu bora ya magereza yenye ukatili zaidi duniani.

Gereza hili lina wafungwa wasioupungua 700 ambao ni wale walioshindikana na wamefungwa vifungo vya maisha ama vya miaka mingi kufikia 70 hadi 90, kwa kufanya makosa makubwa kama ugaidi na mauaji ya watu wengi, lilianza kufanya kazi hiyo ya kuchukua wafungwa wakatili zaidi Novemba, 2000.

Hadi sasa hakuna mfungwa aliyewahi kutoroka ama kutoka kwenye gereza hilo hatari ambalo sheria zake zinashangaza.

Kupitia makala iliyofanywa na televisheni ya National Geographic ilielezwa wafungwa wakishaamka saa 12:00 asubuhi hawatakiwi kulala au kukaa hadi muda wa kulala unapofikia, hali inayowafanya kusimama kwa saa zisizopungua 16 kwa siku.

Pia kila baada ya dakika 15, maaskari husika huwatembelea wafungwa wote, ikiwa ni sehemu ya kupiga doria na kuwatazama na muda wote huwa wanaangaliwa kupitia kamera maalumu zilizofungwa kwenye vyumba vyao.

Kwa siku wafungwa hao hutolewa kwa dakika 90 kwenye selo zao kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi katika eneo maalumu lililotengwa. Wakishamaliza mazoezi hawatoki tena nje na badala yake hukaa ndani hadi kesho yake.

Wakati wanatolewa askari huingia kwenye selo zao na kufanya ukaguzi, ili kuona ikiwa kuna vitu vyovyote wameficha ambavyo haviruhusiwi.

Kwenye gereza hilo wafungwa hawaruhusiwi kutembea wakiwa wamesimama, muda wote hutakiwa kuinama pale wanapotolewa kwenye selo zao.

Wakati mfungwa anatolewa kwenye chumba chake nje huwa kuna askari zaidi ya watano ambao wengine huwa na mbwa, wakiwa tayari kwa ajili ya kukabiliana naye ikiwa atafanya shambulio lolote.

Pia kwenye makala hiyo wafungwa walionekana kuzibwa macho walipokuwa wanatolewa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, lengo likiwa wasijua namna gereza hilo lilivyo na mwishowe wakapanga mpango wa kutoroka.

Hata hivyo, kutoroka pia ni ngumu kwa sababu kila selo ya mfungwa ina milango mitatu ya chuma, ambayo kwa mbele imeweka kitobo kidogo kwa ajili ya kumpenyezea chakula.

Wafungwa kwenye gereza hilo hawarusiwi kuangalia televisheni, kitu pekee wanachoweza kuwa nacho ni redio, vitabu na magazeti.

Kwa siku, wafungwa hulishwa mara nne na hiyo huwa ni supu na mkate tu, hutakiwa kula kwenye selo zao kwa sababu hakuna kantini kwenye gereza hilo.

Denis Avsyuk, mmoja kati ya walinzi wa gereza hilo ameliambia National Geographic kuwa, "Makosa makubwa ambayo wameyafanya watu wanaoletwa hapa huwa ni mauaji, ugaidi, wanaolawiti na kunyanyasa watoto wadogo. Kuwapa cheo cha kuwaita ni watu ulimi wangu unakataa." amesema askari huyo na kuongeza hajawahi hata siku moja kuwaonea huruma.

Mmoja kati ya watu maarufu waliowahi kufungwa kwenye gereza hilo na kupoteza maisha akiwa humo ni mwigizaji kutoka Ujerumani, Carola Neher aliyefariki mwaka 1942.

Ili kuwa askari unayelinda gereza hilo, lazima uwe umepokea mafunzo maalumu na kupata ufaulu wa juu kwa sababu aina ya wafungwa wanaopatikana humo  ni wakatili na wenye uwezo mkubwa wa kiakili na kupigana pia.

Ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa na Serikali ya Marekani mwaka 2012, ilieleza kwamba gereza hilo ni moja kati ya magereza yanayovunja haki za binadamu kwa wafungwa kupigwa, kuchomwa na vitu vya ncha kali na kufungwa minyororo pale wanapofanya makossa, jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu.

Hata hivyo, Russia haikuwahi kutoa taarifa yoyote juu ya kupinga tuhuma hizo, ingawa mwaka 2017, televisheni ya taifa ya nchi hiyo iliachia makala iliyokuwa inaonyesha hali ya gereza hilo na kudai mbali ya mambo wanayofanyiwa wafungwa, bado wana furaha na wamekuwa wakijitahidi kuwa wema.

Pia kwenye makala hiyo ilionyesha kwa sasa wafungwa wanaruhusiwa kufanya kazi ndani ya gereza hilo na kuna kanisa wanaruhusiwa kufanya ibada.

Hata hivyo, watetezi wa haki za binaadamu wanadai video hiyo ni sehemu ya propaganda na hali haipo hivyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Moscow Times, Russia ni moja kati ya nchi zenye magereza mengi duniani, ingawa hakuna hesabu kamili ya kiasi gani wanawekeza kwa mwaka, lakini kiasi kikubwa cha fedha kinadaiwa kutumika kwenye gereza la Black Dolphin kwenye uendeshaji wake.

Pia fedha hizo mara nyingi huchukuliwa kwenye faida zinazopatikana kwa kazi zinazofanywa na wafungwa mbalimbali nchini humo na ripoti ya jeshi la magereza la nchi hiyo Federal Penitentiary Service of Russia (FSIN), ya mwaka 2022, ilieleza kwamba Russia ilipata dola milioni 192 (Sh487 bilioni) kama faida kutokana na kazi zilizofanywa na wafungwa hao.

Wasikie wafungwa wenyewe

Mfungwa mmoja, Nikolai Astankov aliyeiua familia yake yote, kisha miili akaichoma moto msituni, ameliambia National Geographic: "Ikiwa unafikiria mara kwa mara juu ya eneo hili, jibu unalolipata ni kwamba hauwezi kuwa huru hata ikiwaje, kamera zinakumulika muda wote kwenye selo yako, pia kuna mwanga na sensa maalumu ambazo zinagundua miondoko yako na walinzi wanakutembelea kila baada ya dakika 15, kuhakikisha unafuata sheria kila wakati."

Cannibal Vladimir Nikolayev, mmoja wa wauaji maarufu nchini Russia akikumbukwa ka tukio lake la kuuwa mtu, kisha akamkata kata na kuchemsha nyama yake na kuila, pia amefungwa katika gereza hilo.

Lilivyoanzishwa

Kuanzia miaka ya 1800 hadi 1917, nchini Urusi kulikuwa na utawala wa Kifalme uliotambulika kama Russian Empire,

Yemelyan Pugachev alikuwa mmoja ya vijana waliodhamiria kuuangusha utawala huo na kupitia utajiri wa fedha aliokuwa nao aliutumia kama ushawishi wa kuwaaminisha watu kwamba yeye alikuwa Mfalme Peter 11, ingawa ilikuwa ni uongo.

Alikusanya kundi kubwa la wakulima na raia kuendesha maandamano ya kupinga utawala huo, ili kumpindua mfalme kuanzia mwaka 1770 hadi 1774, lakini hilo halikufanikiwa, kwani walikamatwa na kupigwa sana na mwishowe Yemelyan Pugachev akakamatwa na Januari 1775 aliuwawa kwa kukatwa kichwa, kisha mwili wake ukabaluliwa na kukatwa vipande vipande.

Wakati waasi hawa wanapambana kutaka kuupindua ufalme, ndio mwaka 1773, likajengwa gereza hili ili waliokamatwa kwenda kukaa hapo.