Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyejaribu kumpindua Rais Putini afariki ajalini

Kiongozi wa Wagner, Yevgeny Prigozhin ni miongoni mwa abiria 10 waliofariki katika ajali ya ndege iliyoanguka nchini Urusi na kuwaua wote.

Inaaminika kuwa kiongozi huyo alikuwa ndani ya ndege hiyo.

Yevgeny Prigozhin alikwama kumpindua Rais wa Russia, Vladimir Putin mapema mwezi Juni ambapo alikuwa anaongoza kundi Wagner lililojipambanua kulinda masilahi ya Russia kukabiliana na watu wanaoipinga, ikiwemo nchi ya Ukraine.

Hapo awali, kituo cha Telegram kilichounganishwa na Wagner, Gray Zone kiliripoti kwamba ndege hiyo ilidunguliwa na walinzi wa anga katika mkoa wa Tver, kaskazini mwa Moscow.

Prigozhin aliongoza maasi yaliyoshindwa dhidi ya vikosi vya jeshi la Urusi mnamo Juni.


Kwa habari zaidi endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake.