Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaongeza safari za ndege ndani, imo Chato

Muktasari:

  • Serikali imeeleza mpango huo unalenga kufungua nchi na kuongeza safari za utalii.

Dodoma. Serikali imetangaza safari mpya za ndege katika mikoa mbalimbali nchini ambazo zitaanza Juni 2026.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amesema mpango huo unalenga kufungua nchi na kuongeza safari za utalii.

Kihenzile ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mei 25, 2026 wakati akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Chato Kaskazini (CCM) Cornel Magembe ambaye amemtaka Waziri kutangaza lini safari hizo zitaanza rasmi.

Awali katika swali la msingi, Mbunge huyo ameuliza ni lini Serikali itarejesha safari za ndege katika uwanja wa ndege Chato.

Naibu Waziri amesema Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inaendelea kupanua mtandao wa safari kwa kuzingatia upatikanaji wa ndege na mahitaji ya soko.

Amesema kwa sasa, ATCL inahudumia vituo 32 vikiwemo   15 vya ndani ya nchi huku ikikabiliwa na upungufu wa ndege za masafa mafupi na hivyo kushindwa kupanua mtandao zaidi kwa vituo vya ndani kikiwemo cha Geita.

"Serikali inaendelea na mchakato wa ununuzi wa ndege mbili za masafa mafupi zinazotarajia kuwasili mwaka wa fedha 2026/27 zikiwasili, ATCL itaanzisha safari katika uwanja wa ndege Chato,"amesema Kihenzile.

Akitangaza ratiba ya ndege hizo, amesema mapema Juni ndege zitaanza kuruka katika uwanja wa Chato ambako tayari abiria 77 wameshakata tiketi baada ya kutangaza mtandaoni.

Maeneo mengine ambayo ndege zitaanza kuruka ni Sumbawanga ambako usafiri utakuwa Jumatano na Jumapili safari zikianza Juni 10,2026.

"Maeneo mengine ni Mwanza - Dodoma safari zitakuwa Ijumaa na Jumapili kuanzia Juni 5,2026, Kilimanjaro -Mwanza kwa siku za Jumatano na Ijumaa kuanzia Juni 3,2026,"amesema Kihenzile.

Amesema kuanzia Juni Mosi,2026 wataongeza safari za asubuhi  Mbeya na Dar es Salaam, wakati Mkoa wa Arusha kwenda Zanzibar itakuwa Jumatatu, Alhamisi na Ijumaa huku Serikali ikitafakari safari za Musoma na Shinyanga.