Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Petroli, dizeli zashuka bei mwezi Desemba

Muktasari:

  • Kupungua kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia na kushuka kwa gharama za usafirishaji kumetajwa kuwa sababu ya kushuka bei za mafuta nchini

Dar es Salaam. Kupungua kwa bei ya petroli na dizeli katika soko la dunia na kushuka kwa gharama za uagizaji mafuta  kupitia bandari ya Dar es Salaam, Tanga kumetajwa kuwa sababu ya kushuka kwa bei za mafuta kuanzia leo Desemba 6, 2023.

Hiyo ni kwa Mujibu wa taarifa ya ukomo wa bei ya mafuta iliyotolewa jana usiku na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati  Maji (Ewura).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika mwezi Desemba, 2023 bei za mafuta (FOB) kwenye soko la dunia zimepungua kwa wastani wa 0.8 kwa mafuta ya petroli na asilimia 9.11 kwa mafuta ya dizeli.

Pia gharama za kuagiza mafuta kwa Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa wastani wa asilimia 24 kwa mafuta ya petroli na asilimia 30 kwa mafuta ya dizeli huku  Bandari ya Tanga gharama za kuagiza mafuta zikipungua kwa asilimia 30 kwa mafuta ya petroli na asilimia 17 kwa mafuta ya dizeli.

"Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Desemba 2023 yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 8.7  na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 27 kwa petroli na asilimia 23 kwa dizeli.," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Kufuatia kupungua kwa gharama hizo sasa mafuta ya Petroli Dar es Salaam yatauzwa kwa Sh3,158 na dizeli kwa Sh3,226 kwa kila lita kwa bei ya rejareja kutoka Sh3,274 na Sh3,3,74 iliyokuwapo mwezi uliopita.

Kwa upande wa mafuta ya taa ndani ya jiji hilo itasalia kama ilivyokuwa mwezi uliopita yaani Sh3,423 kwa kila lita moja kwa mnunuzi wa rejareja.

Kwa mujibu wa Tangazo hili, bei ya rejareja kwa petroli inakuwa imepungua kwa Sh116 na dizeli kwa Sh148 huku mafuta yataa yakiwa hayana mabadiliko yoyote.

Kwa upande wa Tanga lita moja ya mafuta ya petroli itanunuliwa kwa Sh3,204 huku dizeli ikinunuliwa kwa Sh3,377 kutoka Sh3,274 na Sh3,510 mwezi uliopita mtawaliwa.

Mafuta ya taa katika mkoa huo yatanunuliwa kwa Sh3,469 kwa kila lita.

Kwa watumiaji wa mafuta mkoani Mtwara watatumia Sh3,231 katika kila lita moja ya mafuta ya petroli na Sh3,546 katika kila lita ya dizeli huku mafuta ya taa wakinunua Sh3,495 kwa lita.

"Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika taarifa hii, Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya manyabiashara yoyote atakayekiuka agizo hili, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.