Wizi wa mtandao sasa kuchambuliwa

Muktasari:
Dk Leonard Msele Mtafiti wa Masuala ya Usalama kwenye mitandao wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ( Udom) ndiye anayeongoza kikosi hicho ambacho kinatarajiwa kuanza utafiti huo mapema mwezi huu.
Dar es Salaam. Kikosi kazi cha wafatafiti kimeundwa ili kubaini mbinu zinazoweza kutumika kuwadhibiti watu wanaofanya uhalifu kwa njia ya mtandao ukiwamo wizi na kutunga ujumbe wa maneno ya uzochezi wa siasa na dini.
Dk Leonard Msele Mtafiti wa Masuala ya Usalama kwenye mitandao wa Chuo Kikuu cha Dodoma, ( Udom) ndiye anayeongoza kikosi hicho ambacho kinatarajiwa kuanza utafiti huo mapema mwezi huu.
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Dk Msele aliwataja watu anaotarajia kushirikiana nao katika utafiti huo, Tabo Kondo, Ramadhani Ratis, Hamis Fereji na Leonard Mtembei ambao wote ni wahadhiri wa Udom pia alisema kuna baadhi ya wanafunzi nao watashirikishwa.
“ Tayari tumeshapokea hudi ya Sh100 milioni ili kufanikishwa utafiti huu, ukweli ni kwamba kuna hatari nyingi zilizopo kwenye mtandao’’alisema