Wengi walia na wizi wa mtandaoni

Alishauri kuwapo wataalamu wa ukaguzi wa fedha kupitia mitandao ili kubaini usalama wa fedha na taarifa muhimu zinaweza kuhujumiwa.PICHA"MAKTABA
Muktasari:
Kanembe alisema pamoja na kwamba wizi huo mpya wa kutumia mitandao hauripotiwi, tayari umesababisha upotevu wa zaidi ya dola 80 milioni (Sh1.3 bilioni) katika nchi za Afrika Mashariki pekee.
Arusha. Imetolewa hadhari juu ya kukithiri kwa vitendo vya wizi wa fedha kupitia mitandao ambao umesababisha hasara kubwa kwa taasisi za fedha, kampuni na hata watu binafsi.
Hadhari hiyo ilitolewa jana na Rais wa Taasisi ya Usalama wa Mitandao nchini (Isaca), Boniface Kanembe katika mkutano wa kimataifa wa kuelimisha jamii juu ya hatua za kiusalama za kudhibiti wizi mitandaoni.
Kanembe alisema pamoja na kwamba wizi huo mpya wa kutumia mitandao hauripotiwi, tayari umesababisha upotevu wa zaidi ya dola 80 milioni (Sh1.3 bilioni) katika nchi za Afrika Mashariki pekee.
Alishauri kuwapo wataalamu wa ukaguzi wa fedha kupitia mitandao ili kubaini usalama wa fedha na taarifa muhimu zinaweza kuhujumiwa.
Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Pereira Ame Silima alisema ili kudhibiti uhalifu huo, ni muhimu kuchukua hadhari kwa wadau wote na hasa kujifunza mbinu za kisasa kudhibiti wizi huo.